Afya

Anosmia: Utafanya nini ukijipata umepoteza uwezo wako wa kuhisi harufu?

Anosmia: Utafanya nini ukijipata umepoteza uwezo wako wa kuhisi harufu?

Afya
Utafanya nini ukiamka siku moja ujipate umepoteza uwezo wako wa kuhisi harufu ya kitu chochote? Ni harufu gani utakayoikosa zaidi maishani? Pengine huenda kwa mfano ukatamani kusikia harufu ya marashi mazuri yanayo pakwa na mtu unayependa, harufu ya maua katika bustani au harufu ya chakula kitamu. Hebu sasa tafakari maisha ya mtu ambaye hajawahi kuhisi harufu ya kitu chochote na wala hajui iwapo kina nuka au kunukia tangu alipozaliwa. Hayo ndio yamekuwa maisha ya Wambui Mwangi, 24 kutoka nchini Kenya ambaye ameishi na tatizo la kutosikia kabisa harufu tangu alipozaliwa. Wamboi anasema maisha yake yamekuwa ya kubahatisha. ''Ni maisha magumu kwa sababu watu hawakuelewi ukiwaambia huhisi harufu. Tatizo langu kubwa ni uwezo wa kung'amua kama kitu kinanukia vizuri au vibaya. M...
Coca-Cola ilivyopata jina lake

Coca-Cola ilivyopata jina lake

Afya, Jamii
Coca-Cola ni moja ya kampuni maarufu duniani, ambayo hutengenezwa soda maarufu ya Coke na vinywaji vingine vya soda. Lakini, ilikuwaje hadi ikawa na jina hilo? Labda umewahi kusikia kwamba Coca-Cola wakati mmoja ilikuwa na kiungo cha kusisimua ambacho kiliwafanya wateja kulipenda sana. Hii ni moja ya vilivyochangia jina lake. "Coca", kwa Kiswahili koka, ni jina la jani la mmea wa koka, moja ya viungo ambavyo mvumbuzi wa kinywaji hicho, mwanakemia wa Atlanta John Stith Pemberton, alichanganya na shira kutengeneza kinywaji chake. Majani ya koka hutumiwa kutengeneza kokeini. Wakati huo, mwishoni mwa karne ya 19, ilikuwa kawaida kwa majani ya koka kuchanganywa na divai na kuwa kinywaji cha kuchangamsha mwili. Kinywaji kipya alichotengeneza Pemberton kilikuwa njia nzuri ya kukwep...
Matumizi ya Bangi: Kinywaji cha Coca-Cola kitakachokuwa na bangi kitalewesha?

Matumizi ya Bangi: Kinywaji cha Coca-Cola kitakachokuwa na bangi kitalewesha?

Afya, Biashara & Uchumi
Kampuni maarufu ya vinywaji ya Coca-Cola ni maarufu zaidi kwa kutengeneza soda, lakini sasa inapanga kufanyia majaribio aina mpya ya kinywaji. Kinywaji ambacho kitakuwa na bangi. Lakini je, kitalewesha? Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa BNN Bloomberg, kampuni hiyo itashirikiana na kampuni mwenyeji ya kutengeneza bangi kwa jina Aurora Cannabis. Lengo kuu la kuwa na kinywaji hicho litakuwa ni kupunguza maumivu na si kuwalewesha watu. Kampuni hiyo bado haijazungumzia hadharani mpango huo lakini imekiri kwamba inafuatilia kwa karibu matukio katika sekta ya vinywaji vyenye bangi. "Kwa pamoja na wadau wengine wengi katika sekta hii ya vinywaji, tunafuatilia kwa karibu ukuaji wa soko la vinywaji vyenye bangi aina ya cannabidiol visivyolewesha kama kiungo katika vinywaji vya kubore...
Usingizi wa pono: Kulala bila nguo kuna hatari zozote?

Usingizi wa pono: Kulala bila nguo kuna hatari zozote?

Afya
Kila mtu huwa ana namna yake ya kulala ambayo anajiona kuwa yuko huru Takwimu zinaonesha kwamba idadi kubwa ya vijana, na hasa Ulaya, huwa hawavai nguo ya aina yoyote ile wanapolala. Je, kuna madhara au manufaa? Unafaa kulala bila nguo? Mtaalam wa usingizi Dkt Nerina Ramlakhan ameambia BBC kwamba kuna faida ambazo mtu anaweza kuzipata akivaa nguo za kulalia wakati anapolala. "Kila mtu ana upekee wake na kila mtu ana namna yake ya kulala ambayo anaona huwa inampa uhuru au raha. Kuna baadhi ya watu hawapendi kulala bila nguo huku wengine huwa hawajali kabisa," Dkt Ramlakhan. Anaongeza kwamba kila mtu huwa anahitaji kiwango cha joto ambacho kwake kinamfanya aweze kulala vizuri, na kwa kawaida huwa chini kidogo ya kiwango cha joto mwilini. Anashauri kuwa kama unavaa nguo wakati ...
Dondoo za Afya ya Uzazi: Fahamu kuhusu AFYA yako

Dondoo za Afya ya Uzazi: Fahamu kuhusu AFYA yako

Afya
Uwiano wa Uzito na Urefu/Body Mass Index (BMI) ni njia nzuri ya kuangalia kama uzito wako upo katika afya njema. BMI hutumika kutathimini hali ya lishe ya mtu yeyote pamoja na mtu anayeishi na VVU & ni muhimu katika kugundua mapema baadhi ya matatizo ya afya. Uzito uliopitiliza unasababisha kuongezeka kwa mafuta kwenye mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na uume kuwa midogo na kupungua uwezo wa kujamiana. Kupungua uwezo wa kufanya ngono kwa wanaume ni ishara mojawapo ya ugonjwa wa moyo na kiharusi (stroke). Matumizi ya vileo kama dawa za kulevya, pombe kupita kiasi, uvutaji tumbaku (sigara) huathiri hamu na uwezo wa mwanaume kuweza kusababisha mimba kwa mwanamke. Mfano uvutaji sigara hupunguza uwezo wa manii kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke kwa 20% Kiribatu...
error: Content is protected !!