Afya

Waziri aomba madaktari wa China kuhudumu miaka miwili

Waziri aomba madaktari wa China kuhudumu miaka miwili

Afya, Jamii, Nyumbani
WAZIRI wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed ameiomba Jamhuri ya Watu wa China kurejesha utaratibu wa madaktari wa nchi hiyo wanaokuja kufanyakazi Zanzibar kukaa miaka miwili badala ya mwaka mmoja wa sasa. Alisema tokea kuanzisha uhusiano wa madaktari wa China kuja Zanzibar mwaka 1965 walikuwa wakikaa kipindi cha miaka miwili, lakini utaratibu huo ulibadilika miaka ya hivi karibuni na hivi sasa wanakaa mwaka mmoja. Waziri huyo alitoa ombi hilo alipokutana na ujumbe wa wataalamu wa afya kutoka mji wa Xuzhou ambao upo nchini kufanya tathmini ya madaktari wanaokuja kufanyakazi Zanzibar katika hospitali ya Abdlala Mzee Mkoani na Mnazimmoja. Aliueleza ujumbe huo kwamba utaratibu wa zamani wa timu za madaktari wa China kukaa miaka miwili ulikuwa unatoa fursa nzuri kwa mada...
Homa ya Dengue yaongezeka Tanzania, mji wa Dar es Salaam unaongoza

Homa ya Dengue yaongezeka Tanzania, mji wa Dar es Salaam unaongoza

Afya, Jamii, Mikoani
Homa ya Dengue inaripotiwa kuongezeka katika miji mbalimbali ya Tanzania, huku jiji la Dar es Salaam likiripotiwa kuongoza kwa idadi ya watu wanaogua maradhi hayo. Mganga Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Mohamed Kambi amesema kuwa, kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, watu 1,901 wamepimwa na kuthibitika kuwa wana homa ya Dengue nchini humo. Profesa Mohamed  Kambi ameongeza kuwa, miongoni mwa wanaougua homa ya Dengue 1,809 kati yao wanatoka jijini Dar es Salaam, Tanga 89,  ambapo mikoa ya Singida, Kilimanjaro na Pwani kila mmoja una mgonjwa mmoja. Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania alisema hayo jana Alkhamisi  wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa, wagonjwa wa mkoani Singida, Kilimanjaro na Pw
Utafiti: Haiwezekani kudhibiti maradhi ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Utafiti: Haiwezekani kudhibiti maradhi ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Afya, Jamii, Kimataifa
Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, haiwezekani kudhibiti maradhi ya Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na yamkini maafa ya ugonjwa huo yakawa makubwa zaidi kuliko yale yaliyoshuhudiwa magharibi mwa Afrika mwaka 2013 na 2016. Ripoti zinaonyesha kuwa, katika miezi ya hivi karibuni kesi za maambukizi ya maradhi ya Ebola zimeongezeka sana na kwamba, hakuna dalili za kupungua maradhi hayo. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kesi mpya 298 za Ebola zilimethibitishwa nchini humo kati ya Aprili 15 na Mei tano mwaka huu. Hayo yanajiri katika hali ambayo, juhudi za kukabiliana na maradhi ya Ebola katika Jamhuri yya Kidemokrasia ya Congo zinakabiliwa na changamoto kubwa ambayo ni mashambulio ya makundi ya wanamgambo dhidi y...
Mkutano wa Wadau Kinachozungumzia Kuepeka na Madhara ya Dawa na Vifaa Tiba

Mkutano wa Wadau Kinachozungumzia Kuepeka na Madhara ya Dawa na Vifaa Tiba

Afya, Jamii, Nyumbani
Wadau wa Dawa na Vifaa tiba wakijadili mwangozo uliotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wenye lengo la kuhakikisha matumizi ya dawa na vifaa tiba havileti madhara  kwa wananchi katika Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe. Wakala Chakula na Dawa imeanza kujadili muongozo maalum uliotolewa na Jumuiya ya  Afrika Mashariki wenye lengo la kuinusuru jamii na athari zitakanazo na matumizi ya dawa ambayo hatimae husababisha madhara mbalimbali kwa wananchi. Hayo yameelezwa na Afisa kutoka Wakala wa Dawa na Chakula Mohammed Omar kwenye Ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe katika kikao cha wadau kinachojadili  hatua zinazofaa kuepukana na madhara ya dawa na vifaa tiba. Amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza Muongozo ambao utawezesha kufuatilia madhara ya dawa
Bunge la A.Mashariki laidhinisha marufuku ya vipodozi vinavyobadili rangi ya mwili

Bunge la A.Mashariki laidhinisha marufuku ya vipodozi vinavyobadili rangi ya mwili

Afya, Jamii, Kimataifa
Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone. Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe. Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe. "Athari za vipodozi vyenye hydroquinone zinaonekanana zimesambaa katika jumuiya nzima ya Afrika mashariki ," alisema Gideon Gatpan, mwanasheria kutoka Sudan Kusini. Chini ya kipengele 81(2) cha mkataba ulioanzishwa na Jumuiya ya Afrika Mashrariki ,unaotambua umuhimu wa nchi wanachama katika kuweka viwango, na vipim...
error: Content is protected !!