Afya

Maajabu ya binti aliyejifungua bila kujua ana ujauzito

Maajabu ya binti aliyejifungua bila kujua ana ujauzito

Afya, Kimataifa
Msichana mwenye umri wa miaka 18, ambaye alizirahi kwa muda wa siku nne baada ya kuumwa kichwa ashangazwa kujikuta amejifungua mtoto wa kike. Ebony Stevenson,kutoka Oldham,hakuwa anajua kama ana ujauzito na alienda kulala kwa sababu alikuwa hajisikii vizuri. Msichana huyo alipelekwa hospital mara baada ya kuonekana amepitiwa usingizi kwa muda mrefu hivyo waliamua kumpeleka kupata huduma ya afya na kubainika kuwa ana ujauzito. Mtoto wake alikuwa amejificha katika mfuko wa uzazi ambao ulikuwa umejificha, jambo ambalo huwa linatokea mara chache. Kati miji miwili ya uzazi, mmoja ulikuwa unaendelea kumfanya dada huyo kuendelea kutoa hedhi huku mji mwingine ukiwa unakuza mtoto. Mji huo wa mimba ulikuwa umekaa katika mgongo jambo ambalo lilisababisha ujauzito usionekan...
Tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi

Tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi

Afya, Jamii, Kimataifa
Wanasayansi kutoka nchini Italia wamegundua chanjo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI "AIDS" (Acquired Immune Deficiency Syndrome / Upungufu wa Kinga Mwilini). Kinga hio imefanikiwa kupunguza mwilini idadi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukımwi "HİV" kwa asilimia 90. Timu ya utafiti huu iliongozwa na Barbara Ensoli ambaye amefahamisha yafuatayo kuhusiana na matokeo ya utafiti huo: Utafiti wao mpaka ulipofikia imethibitika kwamba chanjo waliyoitengeneza imetoa majibu ambayo waliyakusudia, yaani kuwa na uwezo wa kutoa kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi. Na cha zaidi imefanikiwa kupunguza kiwango cha virusi vya Ukimwi kwa asilimia 90. Chanjo hiyo ambayo bado ipo kwenye majaribio inailenga aina maalum ya "protein " ijulikanayo kama HIV-1 Tat. Pro
WHO: Joto linaongezeka duniani, maafa yanazidi

WHO: Joto linaongezeka duniani, maafa yanazidi

Afya, Jamii
Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa duniani, WMO limesema ongezeko la viwango vya joto ni ishara ya wazi ya mabadiliko ya tabianchi ya muda mrefu, huku likisema miaka minne iliyopita viwango vilikuwa vya kipekee. WMO katika taarifa imesema miaka  ya 2015, 2016, 2017 na 2018 imekuwa ya joto jingi ikisema kuwa ni “ishara ya wazi kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaendelea.” Uchambuzi wa WMO  unaonyesha kuwa viwango vya wastani vya nyuzi joto kwa vipimo vya selsiasi kilikuwa ni 1,0 juu ya viwango vya kabla ya miaka ya kuanzishwa kwa viwanda 1850 hadi 1900. Akizungumzia mwenendo wa hali ya hewa, Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas amesema mwenendo wa muda mrefu ni muhimu kuliko uchunguzi wa mwaka mmoja mmoja na kwamba taswira inaonyesha kuwa viwango vya
Shirika la afya duniani latoa onyo nchini Libya

Shirika la afya duniani latoa onyo nchini Libya

Afya, Kimataifa
Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuhusu mashambulizi yanayolenga taasisi za afya nchini Libya. Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na shirika hilo, inasema vitendo vya mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya na taasisi za afya nchini libya vilivyorekodiwa kati ya mwaka 2018-2019 ni zaidi ya 41. Katika taarifa hiyo imeelezwa kwamba mashambulizi hayo yalipelekea vifo vya wagonjwa na wafanyakazi wa afya 6, huku wafanyakazi wa afya 25 wakijeruhiwa. Mwakilishi wa WHO nchini Libya Jaffer Seyyid Husein ametoa wito kwa pande zote zinazohusika na mapigano nchini Libya kukomesha mara moja vitendo  vya mshambulizi vinavyolenga wafanyakazi na taasisi za afya. Alisema vitendo hivyo ni kinyume cha sheria za kimataifa na ni makosa makubwa.
Mgomo wawaathiri wagonjwa hospitali za umma Kenya

Mgomo wawaathiri wagonjwa hospitali za umma Kenya

Afya, Jamii, Kimataifa
Mgomo wa wauguzi ulioanza Jumatatu nchini Kenya katika majimbo kumi na nne, umewaathiri zaidi wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali za umma Hata baada ya Wizara ya Kazi na Wizara ya Afya kuunda jopo kazi la kutatua mgogoro huo, Muungano wa wauguzi nchini humo ungali unasisitiza kuwa hautashiriki mazungumzo ya aina yoyote yenye nia ya kusitisha mgomo huo, kwani unadai umechezewa shere na serikali vya kutosha. Zaidi ya wauguzi elfu nane katika hospitali za umma wanaendelea kushiriki mgomo huo kutaka serikali kuu na serikali za majimbo kutekeleza mkataba wa maafikiano unaowapa wauguzi malimbikizi ya marupuru. Serikali kuu na za majimbo zalaumiwa Na mgogoro huu unatokana na serikali kuu na serikali za majimbo kushindwa kutoa mwongozo wa kutekeleza makubaliano ya kureje...
error: Content is protected !!