Bunge la A.Mashariki laidhinisha marufuku ya vipodozi vinavyobadili rangi ya mwili

Baadhi ya mafuta zenye kemikali ya hydroquinone inayobadili ngozi ya mtu kuwa mweupe zikiwa dukani. Bidhaa hizi zimekuwa maarufu sana Afrika Mashariki

Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limepitisha azimio linalotoa wito wa kuwekwa kwa marufuku dhidi ya watengenezaji na waagizaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni, mafuta na urembo wenye kemikali ya hydroquinone inayobadilisha ngozi kuwa nyeupe.

Hydroquinone ni kemikali inayopatikana katika aina mbali mbali za bidhaa mbali mbali za mwili ambayo kwa kawaida imetengenezwa kwa ajili ya kuifanya ngozi kuwa nyeupe.

“Athari za vipodozi vyenye hydroquinone zinaonekanana zimesambaa katika jumuiya nzima ya Afrika mashariki ,” alisema Gideon Gatpan, mwanasheria kutoka Sudan Kusini.

Chini ya kipengele 81(2) cha mkataba ulioanzishwa na Jumuiya ya Afrika Mashrariki ,unaotambua umuhimu wa nchi wanachama katika kuweka viwango, na vipimo, wabunge wamependekeza Baraza la Mawaziri liundwe kwa ajili ya kuchunguza aina za kemikali zilizopo ndani yabidhaa za urembo kama moja ya viwango vya lazima katika kanda ya Afrika Mashariki.

“Baadhi ya bidhaa hizi huwa zina hadi 6% ya kemikali ya hydroquinone,”alisema mbunge kutoka Uganda Suzan Nakawuki.

Jane Ndagire alitumia mafuta yanayochubua mwili kwenye uso wake kwa miaka kadhaa
Jane Ndagire alitumia mafuta yanayochubua mwili kwenye uso wake kwa miaka kadhaa

Kenya na Rwanda, sawa na Afrika Kusini , Ghana na Ivory Coast , zimekwishaweka hatua za sheria za udhibiti au marufuku ya uagizwaji wa bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone.

Wataalamu wa masuala ya ngozi wanasema Kemikali ya hydroquinone inaweza kusababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe na hata saratani ya ngozi.

Ni rahisi sana kununua bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone kwenye maduka ya baadhi ya nchi nyungi za Afrika, zikiwemo Afrika Mashariki
Ni rahisi sana kununua bidhaa zenye kemikali ya hydroquinone kwenye maduka ya baadhi ya nchi nyungi za Afrika, zikiwemo Afrika Mashariki

Namna hydroquinone inavyobadili ngozi:

  • Katika ngozi ya mwanadamu kuna chembechembe ambazo huitwa melanin.
  • Kemikali ya Hydroquinone inakwenda kuzuia utengenezaji wa melanin.
  • kwenye mwili wako hivyo ngozi kupoteza rangi yake ya asili na ulinzi kutokana na miale ya jua yenye madhara Kazi ya chembe chembe hizi ni kuipa Rangi ngozi yako na kuilinda kutokana ni miale ya jua yenye madhara.
  • Kemikali ya Hydroquinone inakwenda kuzuia utengenezaji wa melanin kwenye mwili wako hivyo ngozi kupoteza Rangi yake ya asili na ulinzi kutokana na miale ya jua yenye madhara.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!