Author: Editor-in-Chief

Bobi Wine amdadisi Balozi kwa nini Uganda ‘inawatesa’ wananchi wake

Bobi Wine amdadisi Balozi kwa nini Uganda ‘inawatesa’ wananchi wake

Siasa
Mvutano baina ya Balozi wa Uganda nchini Marekani, Mull Sebujja Katende, na Mbunge Robert Kyagulanyi ulijitokeza Jumatano, wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha VOA - Straight Talk Africa, mjini Washington, Marekani ambapo mbunge amemdadisi balozi ni kwa nini serikali ya Uganda 'inawatesa' wananchi wake. Wakati wa mahojiano hayo Kyagulani maarufu kama Bobi Wine katika madai yake ameishutumu serikali ya Uganda kwa kuwatesa wananchi akionyesha yeye jinsi alivyoteswa baada ya kukamatwa na kikosi maalum cha kumlinda Rais Museveni, huku kwa upande wake Balozi Katende akisisitiza kuwa Uganda ni nchi inayo heshimu mfumo wa demokrasia, sheria na haki za kibinadamu. Katika mahojiano hayo Balozi Katende, na Mbunge Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, walitofautiana kuhusu hali ya...
Sisitizo la Russia na China kwa ajili ya kukabiliana na ubeberu wa sarafu ya Dola

Sisitizo la Russia na China kwa ajili ya kukabiliana na ubeberu wa sarafu ya Dola

Biashara & Uchumi
Rais Vladmir Putin wa Russia amesema kuwa, Moscow na Beijing zimekusudia kutumia fedha zao za kitaifa katika miamala ya kibiashara, badala ya kutumia sarafu ya Dola ya Marekani, kwa kuzingatia mizozo iliopo kati ya Russia na nchi za Magharibi Rais wa Russia aliyasema hayo baada ya kukutana na Rais Xi Jinping wa China katika kikao cha kiuchumi cha mjini Vladivostok, Russia na kuongeza kuwa, Moscow kama ilivyo Beijing, inaunga mkono kwa dhati kutumiwa fedha zao za kitaifa katika mashirikiano yao ya kibiashara. Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo nchi za Magharibi na baada ya kuibuka mzozo wa Ukraine hapo mwaka 2014, ziliiwekea vikwazo vizito Russia. Aidha katika miezi ya hivi karibuni, serikali ya Marekani katika kutoa radiamali ya tuhuma za uingiliaji wa serikali ya Moscow kati
Kimbunga Florence chatolewa tahadhari Marekani

Kimbunga Florence chatolewa tahadhari Marekani

Kimataifa
Wafanyakazi wakiweka vifaa vyenye nguvu kwenye madirisha ya duka huko Wilmington, Carolina Kusini kabla ya kuwasili kwa kimbunga Florence.REUTERS NEWYORK, MAREKANI RAIS wa Marekani  Donald Trump ametangaza hali ya hatari katika maeneo ya Kaskazini na kusini mwa jimbo la Carolina ambapo pia eneo kubwa la Washington DC limechukua pia tahadhari kufuatia kimbunga Florence. Takribani watu milioni 1.7 wanayahama maeneo yao kwa hiari na wengine kwa amri maalumu ili kuepuka madhara ya kimbunga hicho. Kimbunga hicho kinasafiri kwa kilomita 195 kwa saa,huku mawimbi yake yakienda juu kimo cha mita 25. Kimbunga Florence kinachotajwa kibaya kuwahi kutokea siku ya ijumaa 9leo) kinatarajiwa kuyapiga maeneo ya pwani ya mashariki. Kwa mujibu wa chanzo cha usalama nchini Marekani kwa sasa ku
CUF: Hatumtoi Maalim Seif kugombea urais CHADEMA

CUF: Hatumtoi Maalim Seif kugombea urais CHADEMA

Siasa
Chama cha Wananchi CUF kimesema kimeipokea kwa masikitiko kauli iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Baraza la wazee CHADEMA Hashim Issa Juma ya kuwa chama cha CUF kikivurugika watawapokea wabunge wote kugombea kwa tiketi ya CHADEMA pamoja na kumpa nafasi maalim Seif kuwania urais kwa tiket ya chama hicho. Akizungumza na Waandishi wa habari leo huko katika ofisi za chama cha wananchi CUF Mtendeni Zanzibar, Naibu katibu mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazrui amesema kauli hiyo si kweli na hakuna kikao chochote katika chama chao kilichowahi kujadili kauli hiyo. Akifafanua zaidi Mazrui amesema, kauli hiyo ni kauli ya mtu binafsi na  CUF  ni wadau wakuu wa umoja wa katiba UKAWA na katika umoja huo hakujawahi kuzungumzwa jambo hilo. “CUF haijakata tamaa, bado dharuba ni kali, lakini
Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51

Rais wa Liberia George Weah acheza mechi ya kirafiki akiwa miaka 51

Michezo
George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan - akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City Rais wa Liberia George Weah alicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa nchi yake siku ya Jumanne akiwa na miaka 51. Weah ambaye ni mchezaji wa kwanza wa soka kutoka Afrika kushinda tuzo la mchezaji bora wa Fifa, alicheza dakika 79 kwenye mechi ambapo walishindwa na Nigeria kwa mabao 2-1 nyumbani Monrovia. Liberia ilipanga mechi hiyo ya kirafiki kupumzisha shati namba 14 ambalo lilitumiwa na Weah wakati wa kilele cha taaluma yake. George Weah alichezea Monaco, Paris St-Germain na AC Milan - akikaa muda mfupi Chelsea na Manchester City Mchezaji huyo wa zamani wa AC Milan, ambaye aliapishwa kuwa Rais mwezi Januari, alishangiliwa wakati akitolewa uwanjani wakati wa mabadiliko. ...
error: Content is protected !!