Author: Editor-in-Chief

Makubaliano ya Iran na Russia; kukabiliana na hatua za chuki na vikwazo vya Marekani

Makubaliano ya Iran na Russia; kukabiliana na hatua za chuki na vikwazo vya Marekani

Kimataifa
Serikali ya Russia ina hamu na shauku ya kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan katika uga wa biashara na uchumi. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia ilitoa taarifa rasmi jana  na kutangaza kuwa, katika mazunguumzo ya Sergei Ryabkov, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran yaliyofanyika mjini Tehran, Moscow na Tehran  zimekubaliana kutoa dhamana ya kuendeleza mwenendo wa kibiashara wa pande mbili kwa minajili ya kukabiliana na hatua za chuki na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran. Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia, Moscow imesisitiza katika mazungumzo hayo juu ya kufungamana kwake na makubaliano ya nyuklia ya Iran hasa kwa kutilia maanani umuhimu huu k
KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H

Biashara & Uchumi, Jamii, Kimataifa, Mikoani, Nyumbani, Teknolojia, Updates
REF: MM/OD/E/2018/TO/SE11-077                                                                         11-09-2018 Taarifa kwa Umma, As Salaam A’laykum, KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM – 1440 H Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Allah (S.W) kwa kutujaalia sote tukiwa wazima wa Afya na wale wote waliowagonjwa basi Allah awajaalie siha njema, pia kumtakia rehma mtume wetu Muhammad (S.A.W) pamoja na maswahaba wake, wake zake, jamaa zake na waislamu wote kwa ujumla dunia. Pia tunawaombea ndugu zetu katika imani ambao wametangulia mbele ya haki, Kampuni ya Moyo Media tunayo furaha kusherehekea mwaka mpya wa kiislamu 1440 H, Kwa niaba ya Uongozi wa kampuni, tunawatakia wafanyakazi wetu wote na waislamu duniani kote kheri na Baraka za mwaka 1440 H, Tunakuomba Mungu wet
Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare

Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare

Jamii, Kimataifa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Clemens Dori ameashiria kuenea maambukizi ya kipindupindu kusini magharibi mwa Zimbabwe na kueleza kwamba watu 106 wamelazwa hopsitali ya maradhi ya maambukizi mjini Harare. Mkurugenzi Mkuu huyo wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji wa Harare ameongeza kuwa maafisa husika wameweka usimamizi maalumu katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo na kutuma kwenye maeneo hayo timu za maafisa wa Wizara ya Afya za uchukuaji hatua za haraka. Katika kipindi cha kati ya mwezi Agosti mwaka 2008 hadi Juni 2009 watu 98,596 walipatwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe ambapo 4,369 miongoni
Mamia ya wahajiri wafariki dunia karibu na pwani za Libya

Mamia ya wahajiri wafariki dunia karibu na pwani za Libya

Kimataifa
Zaidi ya wahajiri 100 kutoka nchini za Afrika wamefariki dunia katika kipindi cha siku chache zilizopita baada ya boti zao kuzama katika maji ya bahari ya Mediterania karibu na pwani za Libya. Wahajiri hao waliokuwa wakisafiri kutokea Libya kuekelea nchi za Ulaya walikuwa wameabiri kwenye boti mbili, lakini katikati ya safari boti hizo zilipinduka na kusababisha watu hao kughariki baharini. Shirika la Kimataifa la Uhajiri lilitangaza mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu kuwa njia ya baharini ya kutoka Libya kuelekea Italia ni njia hatari zaidi kwa wahajiri wa Kiafrika ambapo tangu ulipoanza mwaka huu wa 2018 wahajiri zaidi ya 1,500 wamefariki dunia katika njia hiyo. Aidha katika kipindi hicho zaidi ya wahajiri haramu 7,000 wamerejeshwa nchini Libya. Wahajiri kutoka nchi za Afrika wa
Rais wa Uganda Yoweri Museveni anataka nchi za nje kukoma kuingilia maswala ya ndani ya nchi yake akisema hatua hiyo ni ukosefu wa maadili na heshima.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anataka nchi za nje kukoma kuingilia maswala ya ndani ya nchi yake akisema hatua hiyo ni ukosefu wa maadili na heshima.

Kimataifa
Rais wa Uganda Yoweri Museveni anataka nchi za nje kukoma kuingilia maswala ya ndani ya nchi yake akisema hatua hiyo ni ukosefu wa maadili na heshima. Museveni, anataka watetezi hao wa haki za binadamu kuacha kumkosoa akitishia kuwafukuza Uganda. Rais pia anataka mashirika ya kutetea haki za binadamu kukoma kukosoa utawala wake, akisema kama wanataka kazi ya kutetea haki za kibinadamu, waende nchi kama Somalia ambapo mfumo wake wa utawala sio thabiti. Katika hotuba yake kwa taifa, Museveni alikosoa wito wa wapinzani wake na watetezi wa haki za kibinadamu, wanaotaka mataifa ya nje kusitisha msaada kwa Uganda, kutokana na madai ya dhulma dhidi ya wapinzani wake. Wanasiasa wa upinzani, pamoja na mawakili wa mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, wanataka Ma...
error: Content is protected !!