Author: Editor-in-Chief

Jamii hii ‘humfunga’ mtoto wa kike kupitia tambiko ili kumzuia kupata mimba punde tu msichana anapoanza kupata hedhi

Jamii hii ‘humfunga’ mtoto wa kike kupitia tambiko ili kumzuia kupata mimba punde tu msichana anapoanza kupata hedhi

Afya, Jamii
Katika jamii ya Pokot kaskazini magharibi mwa Kenya, upangaji uzazi kwa watoto umekuwa ukifanywa tangu jadi. Jamii hii 'humfunga' mtoto wa kike kupitia tambiko ili kumzuia kupata mimba punde tu msichana anapoanza kupata hedhi. Baba hushirikiana na mama ili kujua kama msichana ameanza kupata hedhi na kwa pamoja wanafanya tambiko hilo kwa siri bila msichana kujua. Elizabeth Ndotuch anasema alifungwa na wazazi wake bila kujua, na anaamini kwamba njia hiyo hufanikiwa. "Baada ya kuolewa na kuishi kwa muda, babangu alitumana mimi na mume wangu twende nyumbani. Tulipofika wakaandaa sherehe, wakanifungua... kumbe walinifunga na sikuwa najua." Wanaume huhusika pakubwa katika kufanikisha utamaduni huu. "Mama anaposema mtoto ameanza kupata hedhi, tunaungana na kutafuta wanawake ...
Kampeni za uchaguzi wa rais Madagascar zamalizika

Kampeni za uchaguzi wa rais Madagascar zamalizika

Kimataifa, Siasa
Wagombea urais Madagascar wamemaliza kampeni zao leo huku upigaji kura ukitazamiwa kufanyika Jumatano tarehe saba. Uchaguzi wa mara hii utashuhudia marais watatu wa zamani wakiwania wakiwani fursa ya kuiongoza tena nchi hiyo. Uchaguzi Madagascar unafanyika huku nchi hiyo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya migogoro ya kisiasa. Mgogoro wa karibuni kabisa  ni ule wa mwanzoni mwa mwaka huu baada ya rais Hery Rajaonarimampianina kutaka kubadili sheria za uchaguzi. Rajaomarimampianina atachuana na rais wa zamani Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina ambao kwa nyakati tofauti waliongoza taifa hilo kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi na maandamano. Wikendi hii, vigogo hao watatu wa siasa za Madagascar, ambao ni marais wa zamani wa nchi hiyo waliendesha kampeni zao ambazo zimemalizika
Umoja wa Ulaya washutumu ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania

Umoja wa Ulaya washutumu ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania

Kimataifa, Mikoani, Siasa
Umoja wa Ulaya unasema umemuita mjumbe wake nchini Tanzania kwa mashauriano pamoja na kutathmini upya uhusiano wake na nchi hiyo kutokana na kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania. Taarifa ziliibuka mwishoni mwa juma nchini Tanzania kwamba mjumbe wa Umoja wa Ulaya nchini humo, Balozi Roeland van de Geer, ameitwa kurudi nyumbani Brussles Ubelgiji. Gumzo kubwa limekuwepo kuhusu operesheni ya kuwasaka na kuwachukulia hatua wapenzi wa jinsia moja iliyo idhinishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda inayoanza rasmi leo Jumatatu tarehe 5 Oktoba. Makundi ya kutetea haki za binaadamu yameikosoa operesheni hiyo kwa kukiuka haki za kimataifa za binaadamu. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International lilieleza kwamba kampeni hiyo itashi...
Treni ya umeme kuanza mwakani Tanzania

Treni ya umeme kuanza mwakani Tanzania

Biashara & Uchumi, Mikoani
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema mwaka ujao treni ya kwanza ya umeme itaanza safari baada ya kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge). Amesema utekelezaji wa mradi wa reli hiyo inayoanzia bandari ya Dar es Salaam hadi mji mkuu Dodoma na baadaye hadi nchi za jirani za Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umekamilika kwa asilimia 30. Akizungumza leo wakati akielezea miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya tano tangu Rais John Magufuli alipoingia madarakani, Dk Abbas alisema ujenzi wa reli hiyo ni kati ya mafanikio makubwa ambayo wengi hawakuamini kama yanawezekana kwa kutumia mapato ya ndani “Katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli Serikali imesimama kwenye baadhi ya mambo makubwa ambayo wengi walidhani haiwezekani, tumeahidi
Iran yasema vikwazo vya Marekani ni vita vya kiuchumi

Iran yasema vikwazo vya Marekani ni vita vya kiuchumi

Biashara & Uchumi, Kimataifa, Siasa
Iran imepokea kurejeshwa kwa vikwazo dhidi yake na Marekani kwa kufanya mazoezi ya jeshi la anga. Rais wa Iran Hassan Rouhani amekiri kwamba taifa lake linakabiliwa na kile alichokiita ‘hali ya vita vya kiuchumi” hatua ambayo inaongeza mvutano baina ya Marekani na Iran. Vikwazo hivyo vinamaliza mafao yote ya kichumi ambayo Iran ilipata baada ya makubaliano ya mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 na mataifa makubwa duniani. Wachambuzi wa kisiasa wanasema kuwa vikwazo vipya vya Marekani vitaumiza zaidi sekta ya mafuta ya Iran, ambayo ni muhimu kwa nchi hiyo katika kuinua uchumi wake. Sarafu ya Iran imepungua thamani kwa kiwango kikubwa na kusababisha bei za bidhaa muhimu nchini humo kupanda kwa kasi.   CHANZO: VOA
error: Content is protected !!