Author: Editor-in-Chief

Shamsi ashauri wakandarasi kuacha tamaa

Shamsi ashauri wakandarasi kuacha tamaa

Biashara & Uchumi, Nyumbani
MWENYEKITI wa Kamati teule ya kuchunguza majengo ya skuli 19 za sekondari, Rashid Makame Shamsi, amewashauri wakandarasi wanaopewa kazi na serikali kuacha tamaa na maslahi binafsi badala yake wajali maslaji ya wananchi. Aliyasema hayo wakati akifanya majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo, katika kikao cha baraza la wawakilishi,Chukwani. Alisema kampuni nyingi zinazopewa kazi na serikali zinafanya ubadhirifu jambo ambalo linasababisha hasara kwa serikali. Hata hivyo, alishauri wizara kuwachukulia hatua wote waliobainika kuhusika katika  ubadhirifu. Alisema serikali inawaamini wakandarasi lakini wameshindwa kujiaminisha kwani wanavunja masharti ya mikataba jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya nchi. Sambamba na hayo, kamati hiyo  imependekeza wakala wa ...
Watetezi wa haki za binadamu waandamana kupinga hukumu za vifo Misri

Watetezi wa haki za binadamu waandamana kupinga hukumu za vifo Misri

Kimataifa
Watetezi wa haki za binadamu wamefanya maandamano katika nchi kadhaa duniani kupinga utekelezaji wa hukumu ya kifo dhidi ya wapinzani wa serikali ya Misri. Wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu katika miji ya Tunis na Berlin walikusanyika katika miji hiyo wakilaani hukumu ya kifo iliyotekelezwa nchini Misri dhidi ya wapinzani wa mapinduzi ya serikali halali ya nchi hiyo katika kadhia inayojulikana katika vyombo vya habari kuwa ni ya mauaji ya aliyekuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo, Hisham Barakat. Waandamanaji hao wanasema hukumu za vifo dhidi ya wapinzani hao hazikutegemea misingi sahihi na ya kiadili ya mahakama. Waandamanaji hao ambao walikusanyika mbele ya ubalozi wa Misri mjini Tunis, Tunisia wametoa nara dhidi ya utawala wa kijeshi wa Misri na ...
Dk. Shein amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuitumia mikusanyiko mbalimbali ikiwemo ijitmai, kuhubiri mambo ya kheri katika jamii.

Dk. Shein amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuitumia mikusanyiko mbalimbali ikiwemo ijitmai, kuhubiri mambo ya kheri katika jamii.

Jamii, Nyumbani
Balozi Seif akiifungua Ijitimai ya Kimataifa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar hapo katika Msikiti Mkuu wa eneo la ijitimai hiyo Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al Hajj Ali Mohamed Shein amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuitumia mikusanyiko mbalimbali ikiwemo ijitmai, kuhubiri mambo ya kheri katika jamii. Dk. Shein alisema si katika jambo zuri jamii ya kiislamu kuandamwa na migogoro, hivyo ni vyema wakadumisha mapenzi baina yao ili kuleta ustawi mzuri katika jamii ambao utahakikisha amani na utulivu unakuwepo. Al Hajj Shein alieleza hayo jana katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akiifungua ijitmai ya kimataifa inayofanyika katika kijiji cha ...
Sisitizo la Umoja wa Mataifa la kusaidiwa kifedha Waislamu wa jamii ya Rohingya

Sisitizo la Umoja wa Mataifa la kusaidiwa kifedha Waislamu wa jamii ya Rohingya

Jamii, Kimataifa
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutolewa misaada ya kifedha kwa ajili ya Waislamu wa jamii ya Rohingya walioko nchini Bangladesh. Umoja wa Mataifa umetangaza katika ripoti yake kwamba, unahitajia msaada wa kiasi cha dola bilioni moja kwa ajili ya kuwapatia misaada ya kibinadamu zaidi ya Waislamu 900,000 wa jamii ya Rohingya walioko katika kambi za wakimbizi katika mpaka wa Myanmar na Bangladesh. Umoja wa Mataifa umewahi kusema katika moja ya ripoti zake kwamba, muamala wa serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu Warohingya kuwa ni jinaii dhidi ya binadamu na kutaka kupandishwa kizimbani makamanda wa jeshi wa nchi hiyo wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kizazi dhidi ya Waislamu Warohingya. Waislamu wa Rohingya wakiwa katika maisha ya ukimbizini Hata hivyo ser...
SMZ imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia.

SMZ imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia.

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Mohammed Salum SERIKALI imesema bado ina fursa ya kukopesheka kwa vile ipo katika kiwango cha chini cha kupewa mkopo katika mabenki ya dunia. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Khalid Mohammed Salum, aliyasema hayo jana wakati akitoa majumuisho ya ripoti ya kamati ya kudumu ya bajeti ya baraza la wawakilishi kwa mwaka wa fedha 2018/2019, katika ukumbi wa baraza hilo, Chukwani. Ripoti hiyo, iliyowasilishwa na Mwakilishi wa jimbo la Mpendae, Mohamed Saidi Dimwa, ilifahamisha kwamba deni la taifa hadi kufikia Febuari 2019, ni shilingi 444.480 bilioni linalojumuisha deni la ndani la shilingi 162.870 bilioni na deni la nje shilingi 281.601 bilioni. Mwakilishi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, alisema sababu za kuwepo kwa deni la ...
error: Content is protected !!