Author: Editor-in-Chief

Ilhan Omar asisitiza kurejea White House katika makubaliano ya JCPOA

Ilhan Omar asisitiza kurejea White House katika makubaliano ya JCPOA

Kimataifa, Siasa, Teknolojia
Mbunge Muislamu katika baraza la wawakilishi la Marekani amesema kuwa Washington inapasa kurudi kwenye meza ya mazungumzo na katika makubaliano ya nyuklia na Iran. Ilhan Omar ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa Washington inapasa kurudi kwenye meza ya mazungumzo  na katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. Mbunge huyo katika baraza la wawakilishi la Marekani ameeleza kuwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo hakupasa kujito katika makubaliano hayo ya nyuklia na Iran. Kuanzia Mei nane mwaka huu baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo ya nyuklia na kuanza kutekeleza vikwazo vyake vya upande vyake vya upande mmoja dhidi ya Tehran; Iran nayo imechukua hatua za kusimamisha baadhi ya hatua zake kuhusu makubaliano hayo ya nyuklia na kuto...
RC kuwashughulikia wazee watakaozembea malezi ya watoto

RC kuwashughulikia wazee watakaozembea malezi ya watoto

Jamii, Nyumbani
SERIKALI ya Mkoa wa Kusini Pemba, imesema kuanzia sasa, baada ya mtoto kudhalilishwa yataangaliwa mazingira na kama yataonyesha mzazi amezembea kwenye malezi ataanzwa yeye kuchukuliwa hatua za kisheria kabla ya kutafutwa mtuhumiwa. Alisema wapo baadhi ya watoto hubakwa au kulawitiwa kwa sababu tu ya uzembe wa wazazi, ikiwemo kuwaachilia muda mkubwa nje hasa nyakati za usiku. Mkuu wa Mkoa huo, Hemed Suleiman Abdalla alisema wapo watoto wamekuwa wakiranda randa ovyo nje ya nyumba zao, kwa kwenda kwenye masomo ya ziada, huku wazazi wakiwa hawana ushughulikiaji na kisha hapo hujitokeza wahalifu kuwadhalilishaji. Hemed alitoa karipio hilo hivi karibuni mjini Chakechake, alipokuwa akizungumza na masheha, wanaharakati wa kupamba na udhalilishaji kwenye uzinduzi wa mradi wa...
Ushahidi kuhusu shambulio dhidi ya meli za mafuta unashabiana na kadhia ya silaha za maangamizi ya umati za Iraq

Ushahidi kuhusu shambulio dhidi ya meli za mafuta unashabiana na kadhia ya silaha za maangamizi ya umati za Iraq

Kimataifa
Luxembourg imeashiria taarifa ya kimakosa iliyotolewa na Marekani na kufananisha ushahidi uliotolewa kuhusu shambulio lililotekelezwa dhidi ya meli za mafuta katika bahari ya Oman na kadhia ya silaha za maangamizi ya umati za Iraq. Jean Asselborn Waziri wa Mambo ya Nje wa Luxembourg ameashiria taarifa ya makosa iliyotolewa na Marekani mwaka 2003 kuhusu silaha za maangamizi ya halaiki na kuunga mkono kufanyika uchunguzi huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu shambulio lililotekelezwa hivi karibuni dhidi ya meli za mafuta katika bahari ya Oman. Asselborn ameongeza kuwa anaamini kuwa jukumu muhimu zaidi la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya ni kuzuia kujiri vita na kuwa wanapasa kutekeleza jambo hilo hii leo.  Naye Sten Blok Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi ames...
Vatican inaangalia uwezekano wa kuwafanya makasisi wanaume waliooa katika maeneo ya mbali ya Amazon

Vatican inaangalia uwezekano wa kuwafanya makasisi wanaume waliooa katika maeneo ya mbali ya Amazon

Jamii, Kimataifa
Kanisa Katoliki limekuja na wazo la kuwafanya wanaume waliooa kuwa makasisi katika maeneo yanayozunguka mto Amazon, barani Amerika Kusini. Maeneo hayo ambayo ni mbali, na yapo katikati ya msitu mnene, yana uhaba mkubwa wa makasisi, na bara la Amerika Kusini lina wafuasi wengi wa Ukatoliki. Iwapo suala hilo litapitishwa, itakuwa ni mabadiliko makubwa ndani ya kanisa hilo kwa kipindi cha miaka 1000. Mabadiliko hayo yamependekezwa kwenye Waraka muhimu wa Mazingira wa Papa - Laudato Si - uliochapishwa mwaka 2015. Katika waraka huo, Papa Francis, ambaye ndiye kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ameandika kuwa, eneo hilo la Amazon linakabiliana na na changamoto ambazo (kuzitatua) "inahitaji mabadiliko ya kimfumo na kibinafsi kwa watu wote, mataifa yote (ya eneo hilo la ...
Mafunzo kupitia Mradi wa Ushawishi na Utetezi wa kukuza upatikanaji wa Ardhi na Rasilimali nyengine kwa wanawake yafanyika Pemba

Mafunzo kupitia Mradi wa Ushawishi na Utetezi wa kukuza upatikanaji wa Ardhi na Rasilimali nyengine kwa wanawake yafanyika Pemba

Jamii, Nyumbani
KATIBU wa Jumuiya ya kupunguza umaskini na kuboresha hali za wananchi Kisiwani Pemba (KUKHAWA), Hafidh Abdi Said akitoa maelezo kwa wanajamii kutoka shehia mbuzini, Ole, Mfikiwa na Ndagoni za Wilaya ya Chake Chake, kupitia Mradi wa Ushawishi na Utetezi wa kukuza upatikanaji wa Ardhi na Rasilimali nyengine kwa wanawake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) MRATIB wa Mradi wa Ushawishi na Utetezi wa kukuza upatikanaji wa Ardhi na Rasilimali nyengine kwa wanawake, Zulekha Mauldi Kheir akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo kwa wanajamii kutoka shehia nne zilizomo ndani ya Wilaya ya Chake Chake, huko katika ukumbi wa Mkataba Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) AFISA mipango kutoka kituo cha Huduma za Sheri Zanzibar Tawi la Pemba, Siti Habib Mohamed akiwasilisha mada ya njia
error: Content is protected !!