Aliyekuwa awe mwafrika wa kwanza kwenda anga za mbali afariki dunia

Mwafrika wa kwanza kupata bahati ya kwenda anga za mbali, afariki dunia kwa ajali ya pikipiki kabla ya kutimiza ndoto yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na familia yake kwa shirika la habari la BBC, Mandla Maseko, askari wa jeshi la anga la Afrika kusini, mmoja wa watu 23 waliopata nafasi kutoka katika chuo cha anga cha Marekani baada ya kuwashinda watu milioni 1 kutoka mataifa 75. Amefariki katika ajali ya pikipiki iliotokea mwishoni wa wiki.

error: Content is protected !!