Aliekuwa RPC mjini akutwa amekufa

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, DCP Aziz Juma Mohammed (pichani)

JESHI la Polisi nchini limepata pigo kubwa, baada ya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Azizi Juma Mohammed (58) kufariki kwa tuhuma za kujinyonga.

Tukio hilo lilitokea jana nyumbani kwake Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mwili wake ulikutwa unaning’inia juu ya mchungwa nyumbani kwake  majira ya alfajiri ya Juni 9, 2019.

Daktari alieufanyia vipimo mwili wa marehemu, Marijani Msafiri kutoka hospitali kuu ya Mnazimmoja,alithibitisha kupokea mwili wa marehemu ambapo alisema taarifa zote zitatolewa na  jeshi la polisi.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi mwili wake ulikabidhiwa kwa jeshi la polisi na baadae kwa jamaa zake kwa maziko ambayo yalifanyika jana makaburi ya Mwanakwerekwe.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan, alithibitisha tukio hilo na kusema uchunguzi zaidi juu ya kifo cha DCP Azizi unaendelea.

Azizi aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali katika jeshi la polisi ikiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar, Abdallah Waziri, amefariki katika hospitali ya Mnazimmoja.

Mungu azilaze roho yake mahala pema peponi, Amiin.

CHANZO: ZANZIBAR LEO

error: Content is protected !!