Al Bashir asisitiza kufungamana na mchakato wa amani Sudan

Rais Omar al-Bashir wa Sudan

Rais wa Sudan amesisitiza kuwa nchi yake inafungamana na kukamilishwa mchakato wa amani nchini humo kabla ya kumalizika mwaka huu wa 2018.

Rais Omar Hassan al Bashir amesisitiza kuwa serikali ya Khartoum inaheshimu suala la kupatikana amani nchini humo na kuyatolea wito makundi yenye silaha kukabidhi silaha zao ili kuzuia kumwaga damu za raia wasio na hatia.

Akizungumza na maafiasa na wanajeshi wa nchi hiyo, Rais wa Sudan amesisitiza juu ya wajibu wa serikali kwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo na kuashiria hatua zilizochukuliwa na serikali kutatua matatizo ya kiuchumi nchini humo na kueleza kuwa: Serikali itakabiliana vikali na wale wote wanaovuruga usalama wa nchi. Serikali ya Sudan mwaka jana wa 2017 ilianzisha mpango wa kukusanya silaha zilizotapakaa miongoni mwa raia lengo likiwa ni kudhibiti mapigano ya ndani.

 

error: Content is protected !!