Air Bus wafanya maonyesho uwanja wa ndege wa Zanzibar

KAMPUNI ya Air Bus iliyotengeneza ndege ya Air Tanzania imefanya maonyesho katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, kupitia ndege ya Air Tanzania na kuhudhuriwa na kampuni mbalimbali za ndege.

Akizungumza baada ya kufanyika maonyesho hayo, Meneja wa uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar, Bukheti Juma Suleiman, alisema, maonyesho hayo yana lengo la kuonyesha uwezo wa ndege zao wanazozitengeneza.

Alisema ni jambo la faraja kuona kampuni hiyo kuchagua uwanja huo kufanya maonyesho yao kwani inadhihirisha kuwa uwanja huu ni bora na inaweza kuwa fursa ya kukuza utalii.

Naye Rubani kiongozi wa ndege ya Air Tanzania, Kassim Suhad, alisema, ndege hiyo ina uwezo mzuri wa kuchukua abiria na tokea kuanza safari zake haijawahi kupata hitilafu.

“Kwa kweli ndege ni nzuri, kwanza hainywi mafuta na tokea kuanza safari zake hakujatokezea hitilafu ya aina yoyote,” alisema.

CHANZO: ZANZIBAR LEO

error: Content is protected !!