Afanya mtihani dakika 30 baada ya kujifungua

Mwanamke mmoja nchini Ethiopia amefanya  mtihani hospitali  dakika 30 baada ya kujifungua 
Almaz Derese , mwanamke mwenye umri wa miaka 21 kutoka mkoa wa Metu nchini Ethiopia  alikuwa na  matarajio ya kufanya mitihani kabla  ya kujifungua , lakini mitahani ya shule za upili nchini Ethiopia iliahirishwa kutokana na mwezi wa Ramadhani.

Almaz Derese  alipatwa na uchungu wa kujifungua Jumatatu muda mchache kabla ya mtihani  huo wa taifa kuanza.

Almaz Derese amesema kuwa kusoma akiwa mjamzito haikuwa tatizo na hakutaka kusubiri baada ya mwaka mmoja ndio afanye mtihani huo.

Alifanya mtihani wa lugha ya kiingereza, hisabati na lugha ya Amhariki akiwa hospitali na kumalizia mitihani iliosalia katika kituo kilichoandaliwa kwa ajili ya mitihani hiyo ya taifa Alkhamisi Juni  13.

Mume wa Derese aliwashawishi wasimamizi wa mitihani  kumruhusu mkewe kufanya mitihani yake akiwa hospitali.

Ni jambo la kawaida nchini Ethiopia mwanamke mjamzito kusimamisha masomo na kurejea shuleni baada ya kujifungua.

error: Content is protected !!