Hanga Ngadinda Mosque Project

Hanga Ngadinda Mosque Project

Updates
We therefore appeal for your generous and urgent support towards our project and pray that you will be rewarded in this world and the hereafter for your contribution. Because Uthman ibn Affan reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “Whoever builds a mosque for Allah, then Allah will build for him a house like it in Paradise.” Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 439, Ṣaḥīḥ Muslim 533 The provision estimate cost for renovation is TZS 983,700,000/= (Updates: February 23, 2019: TZS 775,000 has already been contributed, the remained balance is TZS 982,925,000/=) NOTE: Your donation/Zakkat goes a very long way. We have no staffing or administration costs so every penny you donate goes to the project. DONORS REGISTRATION FORM If you would like to be mentione
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed Azindua Tawi la Benki ya NIC bank Tanzania. Eneo la Mlandege Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed Azindua Tawi la Benki ya NIC bank Tanzania. Eneo la Mlandege Zanzibar.

Biashara & Uchumi, Nyumbani
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dk.Khalid Salum Mohammed akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi  wa Tawi jipya la Benki ya NIC Zanzibar, katika eneo la Mlandege  katika jengo la Muzammil .Zanzibar Benki ya NIC Tanzania imefungua tawi jipya Zanzibar hii leo ikiwa sehemu ya mikakati ya kukuza mtandao wake, kuongeza wateja warejareja na kukuza mfuko wake wa biashara ndogo ndogo. Tawi hili jipya lililopo kwenye gorofa ya chini ya jingo la Muzammil Centre, barabara ya Mlandege linalenga kuhudumia jamii ya wafanyabiashara  wa visiwani, kadiri jamii hio inavyo zidi kukuwa hususan kwenye eneo hilo. Uzinduzi wa tawi hili unafikisha idadi ya matawi ya NIC kuwa 6 ya kiwemo matawi 5 bara na 1  Zanzibar. Tawi hili litakuwa la kwanza Zanzibar kutoa cheki za kidijitali na huduma
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 katıka vıpımo vya ritcher limeıpıga Ecuador

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 katıka vıpımo vya ritcher limeıpıga Ecuador

Jamii, Kimataifa
Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 lımerıpotıwa nchini Ecuador. Taasisi ya utafiti wa kijiolojia ya Marekani USGS, imesema kwamba kitovu cha tetemeko hilo ni kilomita 115 kusini mashariki mwa kijiji cha Palora kilichopo eneo la Morona Santiago. Tetemeko hilo limerıpotıwa kutoka kina cha kilomita 132.4. Hakuna hatari ya Tsunami ıliyotangazwa baada ya tetemeko hilo. Mpaka sasa haijatolewa habari yoyote kama kuna vıfo na uharibifu wa mali kutokana na tetemeko hilo.
ZECO yatangaza mgao wa umeme kisiwani unguja kuanzia Ijumaa February 22,2019

ZECO yatangaza mgao wa umeme kisiwani unguja kuanzia Ijumaa February 22,2019

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la umeme Zanzibar ZECO imesema lipo kwenye mpango wa kutafuta mbinu mbadala Ya kupata umeme wa ziada ili kupunguza usumbufu kwa wananchi pindi umeme mkubwa  wa Tanesco ukikatika kutoka Tanzania bara. Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano kutoka kwenye shirika hilo Salum Abdalla Mohamed  amesema shirika la umeme tanesco hivi sasa litazima umeme na kuanza kutoa kwa mgao bara na visiwani kutokana na kufanya matengenezo kwenye eneo la Ubungo. Amesema kuwa kuanzia leo Ijumaa wananchi wanakuwa wanazimiwa umeme na kupata kwa mgao na hali hiyo itaendelea hadi juni  mwezi wa sita kutakapokamilika matengenezo kwenye eneo linalotengenezwa. Aidha salum amewataka wananchi hususani wafanyabiashara wana
Sudan : Bashir atangaza hali ya dharura, aitisha mjadala wa kitaifa

Sudan : Bashir atangaza hali ya dharura, aitisha mjadala wa kitaifa

Kimataifa, Siasa
Rais Omar al-Bashir Rais Omar el-Bashir wa Sudan Ijumaa amewataka waasi, wanaharakati na vyama vya upinzani kukutana na kufanya mjadala wa kitaifa. Rais pia amezivunja serikali za mitaa na taifa na ataunda serikali mpya baada ya mjadala wa taifa kufanyika. Pia ametangaza hali ya dharura ya taifa kwa kipindi cha mwaka mmoja. Nchini Sudan kumekuwa na maandamano yalidumu tangu Disemba 19, wakati serikali ilipandisha bei ya mkate. Tangu wakati huo, maandamano yameongezeka na kuambatana na vurugu kati ya polisi wa kukabiliana na ghasia na waandamanaji. Maandamano sasa yamegeuka na kuwa ya kutaka rais Omar Al-Bashir kuondoka madarakani. Serikali ya Sudan inasema watu 31 wamekufa kufuatia maandamano hayo, lakini wachunguzi wa kimataifa wa haki za kibinadamu wanasema watu ...
error: Content is protected !!