ZATU wampongeza Rais Shein kwa agizo lake

Chama cha Walimu Zanzibar zatu kimesema  utekelezwaji wa agizo   alilolitoa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein juu ya kulipwa walimu wa Zanzibar malimbikizo yao ya uzowefu wa miaka 30 ya kufanyakazi imewapa hamasa na ari walimu kuzidisha kasi ya kufundisha wanafunzi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wa chama hizo Mussa Omar Tafurwa amesema zoezi la ulipwaji wa madeni ya walimu yameshaanza kulipwa kwa walimu pemba  na kuwaomba watendaji kuzidisha kasi ya ulipaji wa madeni hayo kwa walimu wa unguja ili na wao waweze kufaidika na fedha hizo.

Tafurwa amesema ulipaji huo wa madeni umeleta faraja kwa walimu kwani kazi wanayoifanya ya kuwafundisha watoto ni kubwa na inataka umakini mkubwa hivyo  serikali iyone haja ya kuona umuhimu wa kuwalipa madeni yao wanayodai.

Amesema chama cha walimu zatu kinampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar kwa  kuthamini nguvu na juhudi za walimu na kumuomba azidishe motisha kwa wizara ya elimu kuweza kulipa stahiki zote za walimu wanazodai kwani bado kundi kubwa la walimu linadai fedha na baadhi yao wamesha staafu na wengine kufariki dunia wakiwa wanaidai  serikali.

 

 

 

CHANZO: ZANZIBAR 24

error: Content is protected !!