Wamarekani waandamana Washington kutetea Palestina

Wamarekani waandamana Washington kutetea Palestina

Raia wa Marekani wamefanya maandamano mjini Washington wakipinga mpango wa Marekani dhidi ya Palestina uliopewa jina la “Muamala wa Karne”.

Wanaharakati wanaopinga vita na watetezi wa haki za binadamu walifanya maandamano hayo mjini Washington mbele ya nyumba ya mkwe wa Donald Trump, Jared Kushner.

Maandamano hayo ya kupinga mpango huo wa fedheha wa eti Muamala wa Karne yamefanyika mbele ya nyumba ya Kushner kutokana na ukweli kwamba ndiye anayesimamia utekelezaji wa mpango huo.

Kwa mujibu wa mpango wa kinjama wa Marekani unaojulikana kama “Muamala wa Karne” mji wa Quds utakabidhiwa kwa utawala vamizi wa Israel, wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki ya kurejea kwao na Wapalestina watakuwa na haki ya kumiliki sehemu ndogo tu ya ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.

Kushner na viongozi wa Saudia wakipanga njama dhidi ya Palestina

Wataalamu wa mambo wanaamini kuwa, lengo la Marekani la kupendekeza mpango kama huu ni kuhitimisha kadhia ya Palestina na badala yake kufungua mlango wa nchi za Kiarabu kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Kundi jingine la weledi wa mambo linaamini kwamba, kwa mpango wake huo, Trump analenga kuanzisha harakati ya kuelekea katika mpango wa kuunda dola la Kiyahudi kutoka mto Nile hadi Furati na kuliweka suala la chuki dhidi ya Iran sehemu ya mapambano dhidi ya Israel katika eneo la magharibi mwa Asia.

error: Content is protected !!