Waislamu wa Bosnia wazika mabaki ya wenzao 35 waliouawa Srebrenica

Waislamu wa Bosnia wazika mabaki ya wenzao 35 waliouawa Srebrenica

Maelfu ya Waislamu wa Bosnia Herzegovina wamekusanyika hii leo katika mji wa Srebrenica kuadhimisha miaka 23, tangu yafanyike mauaji mabaya zaidi ya umati katika nchi hiyo ya Ulaya, baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Sambamba na kufanyika maadhimisho hayo, Waislamu hao wameyazika mabaki ya wenzao 35 waliouawa katika mauaji hayo ya umati yaliyotokea kati ya mwaka 1992 na 1995.

Nermin Alivukovic, Rais wa Kamati Andalizi ya Kumbukumbu hizo amesema, Srebrenica ni nembo ya kimataifa ya mauaji ya halaiki, na mauji ya namna hiyo hayafai kushuhudiwa tena katika sehemu yoyote ile duniani.

Itakumbukwa kuwa, miaka 23 iliyopita, Waislamu zaidi ya elfu nane wa mji wa Srebrenica mashariki mwa Bosnia Herzegovina waliuawa kwa umati na Waserbia wenye misimamo mikali.

Mabaki ya wahanga wa mauaji ya halaiki Bosnia

Wanamgambo wa Kiserbia wakiungwa mkono na serikali ya Belgrade, waliuvamia mji wa Srebrenica licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulitangaza eneo hilo kuwa la amani mwaka 1993 na kutumwa askari wa umoja huo katika mji huo.

Wakati wa mauaji hayo ya kimbari, wanajeshi wa kulinda amani wa Uholanzi waliokuweko katika eneo hilo hawakuchukua hatua yoyote ya kuwalinda Waislamu hao wa Srebrenica.

error: Content is protected !!