Uteuzi

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 61(1) cha Katiba ya zanzibar ya mwaka 1984,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:-
1. Bibi Salama Mbarouk Khatib ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
2. Bwana Rashid Halid Rashid ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
3. Bwana Ayoub Mohamed Mahmoud ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
4. Bwana Idrisa Kitwana Mustafa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini/ Magharibi.
5. Bwana Mattar Zahor Masoud ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 01 Disemba 2020

BOFYA HAPA

CHANZO: TOVUTI YA IKULU ZANZIBAR