Utaratibu wa mazishi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

Habari kuhusu utaratibu wa mazishi ya kipenzi chetu Maalim Seif.
Asubuhi saa mbili wananchi wa Daarus Salaam wataweza kutabaaruk kwa sala ya janaza hapo Masjid Maamour,Upanga.
Kisha,baada  hapo Insha Allah mwili utasafirishwa kuletwa Unguja na  saa nne tutamsalia katika viwanja vya mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Kisha atapelekwa pemba  na saa saba atasaliwa uwanja wa Gombani na baada laasir atazikwa kwao Mtambwe,Wete Pemba
Tunamuomba Mola wetu amghufirie dhambi zake,   amfanyie wepesi katika maisha yake mapya ya barzakh na amjaalie kuwa ni katika watu wa peponi.
Pia tunamuomba Allah awape subra familia yake, sisi wapenzi wake na wazanzibari wote na kila alieguswa na msiba huu.
Ameen Ameen Ameen