TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI – TAASISI YA VIWANGO YA ZANZIBAR (ZBS)

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Na.1 ya 2011.

 

Lengo kuu la kuanzishwa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar ni kuhakikisha kuwa Zanzibarinakua na viwango kwa ajili ya bidhaa na huduma na kusimamia ubora wa bidhaa na huduma hizo. Viwango na bidhaa zenye ubora zinalenga kulinda afya na usalama wa watumiaji pamoja na kukuza uchumi wa Zanzibar na kuhifadhi mazingira ya nchi.

 

Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS) inakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili katika Ofisi yake iliyopo Unguja na Pemba.

Nafasi zenyewe ni kama zifuatazo:-

 

UNGUJA:

 

 1. AFISA UKAGUZI NA UDHIBITI UBORA MSAIDIZI UHANDISI MITAMBODARAJA LA III –Nafasi Tatu

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe mwenyecheti cha ufundi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazikatika ukaguzi wa vyombo vya moto usiopungua miaka miwili kutokakatika Taasisi inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na uwezo wa kugundua tatizo katika mfumo wa gari kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa ya ukaguzi wa magari.

 

 1. AFISA UKAGUZI NA UDHIBITI UBORA MSAIDIZI UJENZI DARAJA LA III –Nafasi Moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Stashahada ya kawaida (Ordinary Diploma) ya Uhandisi majengo au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA UTHIBITI UBORA DARAJA LA II –Nafasi Mbili

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza/Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya sayansi ya Kemia, Biolojia, Chakula, Sayansi ya mazingiraau fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA VIWANGO NGUO (TEXTILE)DARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya nguoau fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA VIWANGO UHANDISI MAJENGO DARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya Uhandisi Majengo au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. •Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA VIWANGO FAMASIA(PHARMACIST)DARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza au Stashahadaya juu au Stashahada ya Uzamili ya sayansi ya Famasiaau fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA VIWANGO UMEMEDARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya Umeme, Elektroniki au fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA VIPIMO NA UGEZI DARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza/Stashahada ya juu au Stashahada Uzamili ya sayansi ya Fizikia, Vipimo au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. MKUTUBI DARAJALA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu au Stashahada Uzamili katika fani ya Ukutubi/Uandishi wa Habariau fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya Ziada

 

OFISI KUU PEMBA

 1. AFISA UKAGUZI NA UDHIBITI UBORA KEMIKALIDARAJA LA II –Nafasi moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza au Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili ya Kemiaau fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya Ziada

 

 1. AFISA UTHIBITI UBORA DARAJA LA II –Nafasi Moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada ya kwanza/Stashahada ya juu au Stashahada ya Uzamili yasayansi ya Kemia, Biolojia, Chakula, Sayansi ya mazingiraau fani inayolingana kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

 1. AFISA UHUSIANO DARAJA LA II –Nafasi Moja

Sifa za muombaji:

 • Awe ni Mzanzibari.
 • Awe na Shahada yaKwanza/Stashahada ya Uzamili/Stashahada ya Juu katika fani ya Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa Habari au fani inayolingana kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
 • Uzoefu wa kazi ni sifa ya ziada.

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI

Muombaji anatakiwa aandike barua ya maombi na kuambatanisha na barua hiyo:

a)Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.

b)Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.

c)Maelezo binafsi ya Muombaji (CV).

d)Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.

e)Picha moja ya Muombaji (Passport size).

f)Majina na anuani za Wadhamini wawili wanaotambulika. g)Anuani rasmi anayopatikana muombaji, barua pepe na nambari ya simu.

MAMBO YA KUZINGATIWA

 1. Muombaji atakaewasilisha “Statement of Result” au “Progressive Report” maombi yake hayatazingatiwa.

 

 1. Muombaji anatakiwa aainishe nafasi moja anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa.

 

iii. Asiwe muajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

 1. Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe moja kwa moja Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Eneo la Viwanda Amani wakati wa saa za kazi.

 

 1. Kwa nafasi za uajiri kwa Ofisi ya ZBS Pemba waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar iliyopo Chake Chake Pemba jirani na Benki ya NMB.

 

 1. Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Jumanne tarehe 18 Agosti, 2020 saa 9.30 alaasiri.

 

vii. Mawasiliano yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali (short listed).

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI MKUU,

TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR,

S.L.P 1136,

ZANZIBAR.

 

Tangazo hili linapatikana pia katika Tovuti ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) ambayo ni www.zbs.go.tz