Thursday, October 6
Shadow

TANGAZO KWA WADAU WA MAENDELEO

TANGAZO KWA WADAU WA MAENDELEO

Ubalozi wa Marekani Tanzania unawatangazia NGOs na Wadau wote wa Maendeleo kisiwani Pemba kuwa imeandaa mafunzo ya siku moja kuhusu jinsi ya kufanya maombi ya ruzuku zitolewazo na watu wa marekani.

Mafunzo hayo yatafanyika American Space Pemba (American Corner Pemba), Maktaba Kuu Pemba, siku ya Jumanne ya tarehe 05/04/2022 kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Mafunzo hayo yatatolewa na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani.

Mafunzo hayo yatatolewa BURE, nyote mnakaribishwa.

Ili kushiriki mafunzo haya, unaombwa kuthibitisha ushiriki wako kwa kuwasiliana na Mratibu wa American Space Pemba kwa simu namba 0777818121 au barua pepe kwa anuani americancornerpemba@yahoo.com

 

IMETOLEWA NA:

Mratibu,

American Space Pemba,

Mtaa wa Chachani.

Chake Chake,

Kusini Pemba