TAMKO LA CHAKE CHAKE PARALEGAL ORGANIZATION – SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2020.

 

TAMKO LA CHAKE CHAKE PARALEGAL ORGANIZATION

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 2020.

Imetolewa na CHAPO                                          

Juni 16, 2020. Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Chake (CHAPO), Inaungana na taasisi za  Serikali na zisizo za Kiserikali zinazotetea haki za watoto  duniani katika  kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika  Juni 16 kila mwaka.

Katika kuadhimisha siku hii yenye kauli mbiu inayosema”  Mifumo rahisi ya upatikanaji wa Haki ya Mtoto ni msingi imara wa kulinda Haki zao”

Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Chake (CHAPO) kupitia Ripoti ya Haki za Binadamu 2016 kimebaini changamoto nyingi ambazo zinadumaza ustawi wa watoto nchini Tanzania. Changamoto hizo ni pamoja na:

 1. Kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kimwili na kingono dhidi ya watoto ambapo kupitia vyombo mbali mbali kama Dawati la kijinsia la Wilaya ya Chake Chake ,one stop center nk vimeripoti kesi za  ubakaji na ulawiti ,
 2. Vitendo vya Ukatili wa kingono kufanywa na watu wa familia husika au watu wa karibu na watoto hao ; asilimia 49 ya vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto vimeripotiwa kufanyika  na  wafanyaji ni  ndugu wa karibu kwa watoto hivyo kupelekea ugumu katika kufuatwa kwa sheria kwani masuluhisho mengi huishia katika ngazi ya familia na wakati mwingine jamii hushindwa kutoa ushahidi kwa kuoneana aibu.(rushwa muhali)
 3. Kuendelea kushamiri kwa ndoa za utotoni; watoto wawili (2) kati ya watano (5) huolewa chini ya miaka 18 na kupelekea kukatisha haki yao ya kupata elimu.
 4. Mimba za umri mdogo /mashuleni: Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) juu ya ongezeko la mimba za umri mdogo barani Afrika imeitaja Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa  bara la Afrika
 5. Vitendo vingi vya kikatili na mateso dhidi ya watoto:  vimeripotiwa na vyombo vya habari   ikiwa ni adhabu kali  zinazokwaza utu wao ikiwa ni pamoja na kuunguzwa kwa moto, kupigwa hadi kupelekea majeraha hata Ulemavuu   kwa wengine kuripotiwa kwa kiasi kikubwa.

 

 1. Ukeketaji: Mbali na takwimu kuonyesha kupungua kwa vitendo vya ukeketaji, bado mila hii potofu imeendelea kurudisha nyuma harakati za kumkomboa mtoto wa kike kutoka katika wimbi la mila potofu.
 2. Huduma hafifu za afya: changamoto katika sekta ya huduma za afya ikiwemo upungufu wa asilimia 51 wa wahudumu wa afya, kukosekana kwa madawa na vifaa tiba kumeendelea kuyumbisha ustawi wa watoto.

Sababu kuu ya kuzidi kuongezeka kwa changamoto hizo ni pamoja na sheria kandamizi kama sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu msichana kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18; serikali kutenga bajeti duni kwenye huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu; umasikini; mila potofu; Imani za kishirikina; uendeshaji mashitaka kucheleweshwa katika vyombo vya utoaji haki; malezi duni kwa watoto; rushwa pamoja na familia na ndugu wa wahanga kujaribu kuficha aibu ndani ya familia.

Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Chake inapendekeza yafuatayo katika kudumisha ustawi wa watoto nchini Tanzania:

 1. Kutambua umuhimu wa kuzingatia haki za mtoto kwa kutowaficha wahalifu wa vitendo vya kikatili dhidi ya watoto na badala yake kuwaibua na kuacha sheria kuchukua mkondo.
 2. Wazazi na walezi kudumisha malezi bora kwa watoto ili kuzuia mmomonyoko wa maadili unaopelekea mmomonyoko wa ustawi kwa watoto.
 3. Jamii kuachana na mila potofu pamoja na Imani za kishirikina zinazokandamiza ustawi wa watoto.
 4. Vyombo vya usimamizi wa sheria ikijumuisha jeshi la polisi na mahakama kuzingatia ustawi wa watoto wakati wa maamuzi na usimamizi wa haki.
 5. Serikali kufanyia marekebisho sheria zote zinazokandamiza ustawi wa watoto ikiwemo sheria ya ndoa ya mwaka 1971.
 6. Serikali kuboresha sera ya elimu kuwezesha watoto wa kike kuweza kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
 7. Serikali kuelekeza nguvu katika kuboresha huduma za kijamii na miundo mbinu ili kumaliza changamoto zinazowakabili watoto maeneo ya mjini na

Mwisho, Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Chake inaamini watoto ni hazina ya taifa lolote lenye dira ya maendeleo hivyo ni wajibu wa kila mmoja kudumisha ulinzi kwa watoto.

 

Imetolewa leo, Jumanne, Juni 16, 2020.