Taarifa kwa vyombo vya Habari – Uteuzi

Taarifa kwa vyombo vya Habari

Kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984,kinachosema kwamba “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa na Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 6 Disemba,2020

 

CHANZO: TOVUTI YA IKULU ZANZIBAR