TAARIFA KWA UMMA NA WADAU WETU WA PEMBA LIVE

KUMBUKUMBU NAMBA: REF: MM/E/2019/TO/AU09-007

Ndugu wateja na wadau,

Amani na Rehma za M/Mungu ziwe nanyi,

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutubariki neema ya afya na uzima hadi sasa.

Pili kwa niaba ya uongozi wa kampuni ya Moyo Media Co. Ltd, tutumie fursa hii kuutarifu umma, wateja na wadau wetu wote wa Pemba Live® kwamba kuanzia leo Ijumaa ya tarehe 09/08/2019 tunasitisha rasmi huduma ya kutoa habari kwa kupitia mtandao wetu wa www.pembalive.info  

Tumeamua kuchukua hatua hii kwa lengo la kuboresha huduma zetu kimtandao, ambapo kuanzia mwezi wa kumi (October 2019) In Shaa Allah, tunatarajia kuanzisha huduma mpya za habari kwa kupitia mitandao mbadala ya Pemba Live®.

Wavuti ya www.pembalive.info kuanzia hivi karibuni itaanza kuhusishwa na utoaji huduma za kimtandao tu kama vile masoko, matangazo mbali mbali yakiwemo ya ajira, matangazo rasmi, orodha za biashara, viungo muhimu vya kimtandao n.k

Na huduma za habari, magazeti mtandao n.k zitatolewa kwa kupitia mitandao mbadala ambayo iko katika matengenezo kwa sasa na tunatarajia itaanza hivi karibuni In Shaa Allah.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa sasa wakati tukiwa tunaboresha huduma zetu. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa admin@pembalive.info

Imetolewa na

Uongozi wa Kampuni,

Moyo Media Co. Ltd