Thursday, October 6
Shadow

Shaibu Foundation yazindua mradi wa elimu mtandao kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba

Ndugu Mustafa Moyo, Raisi wa taasisi ya Shaibu Foundation akizindua mradi wa Elimu Mtandao kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba.

Shaibu Foundation ni taasisi isiyo ya kutengeneza faida iliyosajiliwa Zanzibar, inayojikita katika maeneo mbali mbali ikiwemo elimu.

Siku ya Jumamosi ya tarehe 26/06/2021 Shaibu Foundation ilizindua mradi wa elimu mtandao awamu ya pili kwa skuli za msingi na sekondari kisiwani Pemba. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa American Space Pemba. Mafunzo hayo yatafanyika kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu kwa kila skuli itakayonufaika. Ambapo skuli zitatakazonufaika na mradi huo ni Ng’ambwa Sekondari, Mchanga Mdogo Msingi, Mjananza Msingi, Makoongwe Msingi na Sekondari, Msuka Msingi na Sekondari, Vikunguni Msingi na Sekondari, Chasasa Sekondari, Utaani Sekondari na Chuo cha Kiislamu Pemba.

Ndugu Mustafa Moyo akiwasilisha mada jinsi mradi utakavyotekelezwa

Mradi huu ulianza rasmi mnamo mwaka 2018, ambapo kwa awamu ya kwanza walimu wa Skuli ya Madungu msingi walinufaika na mradi. Kwa kupitia mradi huu, walimu wanufaika watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu elimu mtandao na jinsi inavyofanya kazi.

Baadhi ya walimu wawakilishi wa skuli zitakazonufaika na mradi wakisikiliza kwa makini kuhusu mradi
Baadhi ya walimu wawakilishi wa skuli zitakazonufaika na mradi wakisikiliza kwa makini kuhusu mradi

Aidha Ndugu Mustafa Moyo ambae ni raisi wa taasisi hiyo alifafanunua jinsi mafunzo hayo yatakavyo wanufaisha walimu na skuli shiriki ikiwemo kuziwezesha skuli kufundisha kidijitali kwa kutumia mifumo ya kisasa zaidi inayotumika kote ulimwengu, kuwawezesha walimu kuwa na uelewa zaidi juu ya mifumo ya elimu mtandao, kwaunganisha walimu na fursa mbali mbali za elimu mtandao n.k.

Baadhi ya walimu wawakilishi wa skuli zitakazonufaika na mradi wakisikiliza kwa makini kuhusu mradi