Tuesday, September 28
Shadow

Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema wakati umefika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyakazi kwa karibu na wananchi, ili waweze kutambua umuhimu wa kuwepo Jumuiya hiyo.Dk. Mwinyi amesema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar, alipozungumza na Ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dk. Peter M. Mathuki, uliofika kwa ajili ya kusalimiana. Amesema azma ya Jumuiya hiyo kufanya baadhi ya vikao vyake vya Bunge pamoja na Mahakama hapa Zanzibar, itawafanya wananchi wawe na uelewa wa kuwepo kwa Jumuiya hiyo pamoja na kujenga imani nayo.Aidha, alisema hatua ya Ujumbe huo kukutana na viongozi wa sekta binafsi hapa Zanzibar ni jambo jema, hususan katika uimarishaji wa biashara kwa kuzingatia kuwa wa...
Dk.Hussein Ali Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar kuwashajihisha wawekezaji wa nchi hiyo kuja nchini kuwekeza katika sekta za Utalii, Uvuvi pamoja na mafuta na Gesi.

Dk.Hussein Ali Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar kuwashajihisha wawekezaji wa nchi hiyo kuja nchini kuwekeza katika sekta za Utalii, Uvuvi pamoja na mafuta na Gesi.

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameiomba Serikali ya Qatar kuwashajihisha Wawekezaji wa nchi hiyo kuja nchini kuwekeza katika sekta za Utalii, Uvuvi pamoja na mafuta na Gesi.Dk. Mwinyi ametoa ombi hilo Ikulu jijini Zanzibar, alipozungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Hussain Ahmad Al Humaid, aliefika kujitambulisha.Amesema tayari Zanzibar imeanzisha Sera maalum kwa ajili ya kuendeleza Uwekezaji, ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wake. Rais Dk. Mwinyi aliiomba nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kuisaidia Zanzibar katika uimarishaji wa sekta za Maji, Afya pamoja na elimu.Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizo, na kubainisha umuhimu wa hatua hiyo kuendel...
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake.

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ina dhamira ya dhati ya kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake ili kujenga uchumi imara kwa Taifa.Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo huko katika ukumbi wa Hoteli ya Verde nje kidogo ya Jijini la Zanzibar wakati akifungua Kongamano la siku moja lililobeba mada “Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Uhifadhi wa Mazingira Zanzibar”. Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alieleza kuwa bado kuna fursa, faida na vipaumbele vya uwekezaji zaidi chini ya Uchumi wa Buluu kama vile katika sekta za uvuvi mdogo mdogo, uvuvi wa bahari kuu, ufugaji samaki na mazao ya bahari.Alizitajas Sekta nyengine kuwa ni ukulima wa m...
TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS, MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UNGA 76)

TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS, MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UNGA 76)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS, MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA (UNGA 76) Dodoma, 08 Juni 2021 Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano wa 76 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 76) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 7 Juni 2021, New York – Marekani. Katika uchaguzi huo, Tanzania imepita bila kupingwa ambapo mara ya mwisho Tanzania kuwa Makamu wa Rais ni mwaka 1991. Katika uchaguzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Maldives, Mhe. Abdulla Shahid, amechaguliwa kuwa Rais wa Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 76) kwa kura 143 dhidi ya mpinzani wake Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Dkt. Zalmai Rassoul aliyepata kura 48. Majukumu ya Makamu wa Rais ni kusaidiana na Rais katika ...
PPC waadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Pemba

PPC waadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Pemba

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wamekumbushwa kuwa, iwapo wataandika habari bila ya upendeleo, zinakuwa daraja la kufikia maendeleo ya kweli kwa jamii iliyowazunguruka. Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa kaskazini Pemba Khatib Juma Mjaja, alipokuwa akizungumza na waandishi hao na wadu wao, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Maktaba Chake chake, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, duniani. Alisema, habari ni kichecheo muhimu na adhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii, kwa kule habari hizo zilizoandikwa kwa uweledi watazitumia. Alieleza kuwa, moja ya shaka wanayokumbana nayo jamii, ni kukosa habari za aina zote, kwa kule baadhi ya waandishi wa habari, kuegemea habari za aina moja katika k...