Mlipuko wa Ebola wasababisha vifo vya watu 17 Kongo

Mlipuko wa Ebola wasababisha vifo vya watu 17 Kongo

News Bulletin
Watu 17 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC. Wizara ya afya imesema kuwa kesi 21 za Ebola ziliripotiwa ndani ya wiki tano na kusababisha vifo vya watu 17 katika eneo la Bikoro nchini DRC. Kwa mujibu wa habari hatua za kuudhibiti ugonjwa huo zinaendelea kwani umekuwa ni hatari kwa jamii nzima wakiwemo wafanyakazi. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa la WHO limetuma madaktari kusaidia kupambana na ugonjwa huo.
SMZ yaeka wazi haina mpango wa kuzifanyia matengenezo barabara zilizo chimbika kwa mvua

SMZ yaeka wazi haina mpango wa kuzifanyia matengenezo barabara zilizo chimbika kwa mvua

News Bulletin
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haina Mpango wa Kuzifanyia matengenezo Barabara za Ndani katika mwaka wa fedha 2018/19. Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Naibu Waziri wa Nchi OR tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Shata Shaame amesema barabara hizo hazitofanyiwa matengenezo kutokana na uhaba wa Fedha. Amesema katika kuhakikisha wananchi wananufaika na Miundombinu ya Barabara Serikali itaendelea kutoa maelekezo kwa Serikali za mitaa kuweka kipaumbele chake kufanya matengenezo ya Barabara za ndani ili kuwapunguzia Usumbufu wananchi. Hata hivyo ametoa wito kwa Wawakilishi kushirikiana na Watendaji wa Serikali za mitaa ili kuangalia namna ya kuzifanyia matengenezo Barabara hizo kupitia fed...
Mama wa Jay-Z: Nilimwambia mwanangu nina mpenzi wa jinsia moja

Mama wa Jay-Z: Nilimwambia mwanangu nina mpenzi wa jinsia moja

News Bulletin
Jay-Z alifahamu kuwa mama yake anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja Mama yake mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani, Jay- Z amezungumza namna ambavyo mtoto wake amekuwa akimpa moyo alipomwambia kuwa amekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja Gloria Carter aliiambia hadhira katika tuzo za GLAAD kuwa ni mara ya kwanza kuzungumza na mtu kuhusu ukweli wake Mama wa watoto wanne alitunukiwa tuzo akitambuliwa kwa mchango wake kwenye wimbo uitwao Smile uliotolewa mwaka jana. Alisema: ''Smile imekuwa halisia kwa sababu nilimshirikisha mtoto wangu nikimweleza mimi ni nani.'' ''Mtoto wangu alilia na akasema: 'lazima maisha yalikuwa mabaya sana kuishi namna hiyo kwa muda mrefu.'' ''Maisha yangu hayakuwa mabaya,''aliongeza. ''Nilichagua kuilinda familia yangu.Nilikuwa n...
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI UWEZESHAJI WAZEE WANAWAKE NA WATOTO

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI UWEZESHAJI WAZEE WANAWAKE NA WATOTO

Ajira
Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kama ifuatavyo:- KAMISHENI YA KAZI: 1.Afisa Kazi Mikoa Daraja la II “Nafasi 3” Sifa za Waombaji: •Awe ni Mzanzibari. •Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mahusiano ya Viwanda au Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar 2.Mkaguzi Kazi Mikoa Daraja la II “Nafasi 5” Sifa za Waombaji: •Awe ni Mzanzibari. •Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mahusiano ya Viwanda au Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 3.Mtunza Ghala Daraja la III “Nafasi 1” Sifa za Waombaji: •Awe ni Mzanzibari. •Awe amehitimu Stashahada ya Kutunza Ghala (Store keeper) kutoka katika Chuo k
Walio na upara sasa wana sababu ya kutabasamu: Dawa ya kutibu upara yapatikana

Walio na upara sasa wana sababu ya kutabasamu: Dawa ya kutibu upara yapatikana

News Bulletin
Dawa ya kutibu upara imegunduliwa kwa kutumia dawa ya kutibu mifupa iliodhoofika Watafiti waligundua kwamba dawa hiyo ina athari kubwa katika mashina ya nywele katika maabara kwa kuzipatia nguvu nywele kumea. Dawa hiyo inashirikisha vipengele vinavyolenga protini ambayo hutumika kukatiza umeaji wa nywele na hivyobasi kusababisha upara. Kiongozi wa mradi huo Dkt. Nathan Hawkshaw kutoka chuo kikuu cha Manchester alisema inaweza kuleta tofauti kwa watu wanaokabiliwa na ukosefu wa nywele Ni dawa mbili pekee ambazo hutumika kutibu upara minoxidil, kwa wanaume na wanawake finasteride, kwa wanaume pekee Dawa zote mbili zina madhara na hukosa kufanya kazi mara nyengine hivyobasi waathiriwa hupendelea kufanya upandikizaji wa nywele badala yake Utafii huo uliochapishwa katika ...
error: Content is protected !!