Wito wa Somalia kwa wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika forodha  ya mjini Mogadishu

Wito wa Somalia kwa wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika forodha ya mjini Mogadishu

Biashara & Uchumi, Kimataifa
Somalia inayo matumaini makubwa kufungua forodha  yake ya mjini Mogadishu  kwa kutoa wito kwa wawekezaji wa kigeni. Inafahamika kuwa forodha ya mjini Mogadishu ilikuwa na umuhimu mkubwa katika shuhuli za uchukuzi kati ya eneo hilo la pembe ya Afrika kuelekea katika mataifa tofauti barani Ulaya tangu miaka ya 1960. Hali ilibadilika tangu mwaka 1991 wakati ambapo kulizuka mapigano. Uongozi wa forodha nchini Somalia  baada ya kuona kuwa  usalama unazidi kuimarika umetolea wito wawekezaji kuwekeza katika  sekta hiyo.
Waziri Aboud: Serikali inatekeleza ilani ya CCM

Waziri Aboud: Serikali inatekeleza ilani ya CCM

Siasa
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud, asema serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020, kupitia Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUZA III). Alisema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi ya kusimamia ofisi za viongozi wakuu ya mwaka 2017/2018. Alisema lengo la serikali ni kuona uchumi wa nchi unakua na kupunguza umaskini kwa wananchi wake, hivyo serikali imekuwa ikisimamia ipasavyo sera na ilani hiyo ili kuona lengo hilo linafikiwa. Akizungumzia dawa za kulevya, alisema jumla ya skuli 108 zimepatiwa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Alisema kati ya skuli hizo,...
Askari mwanamke India aliyezuia Mauaji ya WhatsApp

Askari mwanamke India aliyezuia Mauaji ya WhatsApp

Jamii, Teknolojia
Rema Rajeshwari mkuu wa polisi wa Wilaya Polisi waliamua kufanya uchunguzi kwenye simu za wanavijiji waligundua kuwa kati ya video na picha 30 na 35 ambayo iliwakuwa ikisambazwa na kumuonesha mtoto akiwa ametekwa,kwa uhalisia, hiyo ilikuwa ni kutoka katika moja ya filamu kutoka nchini Pakstani ambayo iliondolewa baadhi ya maudhui yake na kisha kufuatiwa na sauti. Jambo lisilo la kawaida latokea muda wa magharibi kwa wanavijiji zaida ya 400 katika mji wa Telangana uliopo kusini mwa India Wanaume na wanawake walirejea majumbani mwao mapema kuliko kawaida kutoka mashambani,wakifunga milango,wakizima taa na kusalia ndani licha ya watoto kuwa na kawaida ya kucheza nje kwa muda mrefu, tulikuwa wa kwanza kurudi,mitaa yote ilikuwa kimya na hofu ikiendelea kutanda. Hii ilikuwa si tabia ya ...
Baraza kuu la UN mbioni kuanza

Baraza kuu la UN mbioni kuanza

Kimataifa
Viongozi takriban 130 wa taifa na serikali wanatarajiwa kuwasili wiki hii mjini New York kuhudhuria hadhara kuu ya Umoja wa mataifa- kongamano linalozungumzia migogoro inayoikumba dunia. Viongozi takriban 130 wa taifa na serikali wanatarajiwa kuwasili wiki hii mjini New-York kuhudhuria hadhara kuu ya Umoja wa mataifa- kongamano linalozungumzia migogoro inayoikumba sayari yetu na ambako makubaliano kufikiwa pembezoni mwa mikutano. Viongozi wa mataifa 193 wanachama wa Umoja wa mataifa wanawakilishwa katika hadhara kuu. Rais wa Marekani Donald Trumpo, sawa na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa watahudhuria huku wengine mfano wa kansela Angela Merkel wa Ujerumani, au Vladimir Putin wa Urusi watawakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya nchi za nje. Haijulikani bado kama rais wa Venezuela ...
error: Content is protected !!