Mugabe ‘anaendelea vizuri’ baada ya kujiuzulu

Mugabe ‘anaendelea vizuri’ baada ya kujiuzulu

News Bulletin
Mpwa wa Robert Mugabe anasema kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe ana raha na afya njema licha ya kulazimishwa kujiuzulu wiki hii baada ya kutawala kwa miaka thelathini na saba. Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, kwamba alimtembelea mjombake ambaye anasema anaendelea vizuri baada ya utimuliwa kwake madarakani. Kauli ya Leo Mugabe inaashiria kiongozi huyo mkongwe amezoea kwa upesi kutimuliwa kwake kutoka uongoai wa taifa hilo. Amesema mjombake anatazamia maisha yake ya baada ya uongozi, ambayo yatajumuisha ukulima na kuishi katika nyumba yake mashambani. 'Grace, bado yupo naye' amesema Leo Mugabe akimaanisha mkewe rais huyo wa zamani. Ameeleza kuwa anashughulika na mipango ya kujenga chuo kikuu kwa heshima ya mumewe ili kuwapa shughuli ya kufanya. Hat...
Uturuki yaomboleza vifo vilivyosababishwa na shambulio la kigaidi Sinai

Uturuki yaomboleza vifo vilivyosababishwa na shambulio la kigaidi Sinai

News Bulletin
    Uturuki yatangaza siku moja ya maombolezo Jumatatu kufuatia maafa yaliotokea Sinai katika shambıulizi lililolenga mskiti wakati wa ibada ya mchana. Watu zaidi ya 300 walifariki katika shambulizi hilo Kaskazini mwa Sinai katika mskiti wa El Ravda. Taarifa hiyo kuhusu siku moja ya maombolezo imetolewa katika tangazo kutoka katika ofisi za waziri mkuu wa Uturuki. Tangazo hilo limefahamisha kuwa bendera za Uturuki zitapandishwa nusu mlingoti kote Uturuki na katika balozi zake kote ulimwenguni Jumatatu. Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım amesema kuwa Uturuki ipo bega kwa bega na Misri katika wakati huu wa majonzi. CHANZO: TRT
Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia yataka kuwa na familia

Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia yataka kuwa na familia

News Bulletin
Roboti iliyopewa uraia nchini Saudi Arabia imesema kuwa ina haki ya kuwa na familia. Roboti hiyo kwa jina la Sophia ilitengenezwa nchini Hong Kong na kupewa uraia nchini Saudi Arabia mwezi uliopita. Roboti hiyo İimesema kuwa ingependa kuwa na familia wakati ilipohudhuria mkutano wa habari ulioandaliwa nchini UAE. Kwa mujibu wa habari roboti hiyo imesema kuwa familia ni kitu muhimu sana. Robot hiyo imesema kuwa kila mwanadamu ana haki ya kuwa na familia na watu wenye hisia sawa na yeye.Jambo hilo ni muhimu sana hata kwa roboti.Aliwaambia wanadamu wajisikie furaha kuwa na familia.
Watoto 20 wafanyiwa upasuaji wa moyo

Watoto 20 wafanyiwa upasuaji wa moyo

News Bulletin
TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart) ya Israel zimefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (catheterization) kwa watoto 20 wenye matatizo ya moyo. Upasuaji huo ambao unatumia mtambo wa cathlab umefanyika katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza Novemba 23 na kumalizika leo. Matibabu yaliyofanyika ni ya kuziba matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo. Taarifa kutoka taasisi hiyo imesema katika kambi hiyo watoto 100 walifanyiwa uchunguzi wa moyo kati ya hao 60 wenye matatizo makubwa watapelekwa nchini Israel kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na 40 watatibiwa nchini. “Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 25, tunaamini hadi kambi itakapomalizika watoto wote hawa watakuwa wamepata matibabu.
Video yafungiwa na Serikali

Video yafungiwa na Serikali

News Bulletin
Video mpya ya kundi la muziki kutoka Kenya Sauti Sol ft Patoranking ‘Melanin’, imefungiwa na serikali ya nchi hiyo chini ya bodi ya filamu Kenya (Kenya Film Classification Board KFCB) Mkurugenzi wa bodi ya filamu Kenya Dr. Ezekiel Mutua, ametoa taarifa rasmi ikieleza kuwa imepokea malalamiko kutoka kwa watu kuwa haina maadili, na imetolewa bila kupitishwa kwenye bodi hiyo kuipa grade. Pamoja na hayo bodi hiyo ambayo inasimamia ubora wa kazi za filamu nchini Kenya imevitaka vyombo vya habari kutocheza video hiyo, hsusan muda ambao watoto wanaangalia television. Video mpya ya Sauti Sol wakimshirikisha Patoranking imeachiwa rasmi Novemba 20 mwaka huu, na mpaka sasa hivi tayari ina zaidi ya viewers laki 3 kwenye YouTube. CHANZO: ZANZIBAR 24
error: Content is protected !!