Madereva walevi kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti Kenya?

Madereva walevi kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti Kenya?

News Bulletin
Mamlaka ya usalama wa uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi. Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani. ''Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria'', alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja. Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini. CHANZO: BBC
Ndege ya jeshi la Marekani yafanya ajali katika kisiwa cha Japan

Ndege ya jeshi la Marekani yafanya ajali katika kisiwa cha Japan

News Bulletin
Ndege ya jeshi la Marekani imefanya ajali ikiwa na watu 11 katika kisiwa cha Japani cha Okinawa katika bahari ya Pasifiki. Waziri wa ulinzi wa Japani Itsunori Onodera amefahamisha kuwa wafanyaki wanane wa ndege hiyo wamepatikana wakiwa salama. Wafanyakazi wengine watatu bado wanatafutwa. Ndege hiyo iliofanya ajali ni aina ya C2 na ilipata ajali ikiwa katika umbali wa kilomita 150 Kaskazini-Magharibi mwa Okinotori-shima Kusini mwa Japan.  
WADAIWA SUGU TTCL KUPANDISHWA KIZIMBANI

WADAIWA SUGU TTCL KUPANDISHWA KIZIMBANI

News Bulletin
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya kampuni ya simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwake na kuwataka kuwachukulia hatua wale wote wanaodaiwa madeni sugu, upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dokta Mary Sassabi. NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa wadaiwa sugu ambao hawafuati taratibu za kulipa madeni wanayodaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) watapelekwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria.   Hayo yalisemwa na Waziri huyo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi makao makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam, akizungumza na Menejimenti ya kampuni hiyo.   Alisema kuw...
error: Content is protected !!