Togo, taifa pekee Afrika launga mkono uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem katika mkutano wa Umoja wa Mataifa

Togo, taifa pekee Afrika launga mkono uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem katika mkutano wa Umoja wa Mataifa

News Bulletin
Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa umepiga Kura ya kutoyatambua maamuzi ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Makubaliano hayo ya mkutano wa umoja wa mataifa yamefikiwa pamoja na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump aliyetishia kuzikatia msaada wa kifedha nchi zote zitakazopinga msimamo wake. Togo ndio taifa pekee barani Afrika kunga mkono uamuzi wa rais wa Marekani na serikali yake kutangaza kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa Israel. Jumla ya wanachama 128 wamepiga kura wakipinga uamuzi wa Trump ktangaza Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Mataifa 35 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hilo hayakuonesha msimamo. Cameroon, Sudan Kusini, Benin, Lesotho, Malawi, Rwanda na Uganda ndio mataifa ya bara la Afrika ambayo hayakuonesha msimamo wao. Canada ...
TUNDURU KUWAPATIA MICHE BURE YA KOROSHO WAKULIMA WAKE

TUNDURU KUWAPATIA MICHE BURE YA KOROSHO WAKULIMA WAKE

News Bulletin
Na Muhidin Amri,    Tunduru. HALMASHAURI ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na bodi ya korosho nchini, imeotesha miche bora ya zao la korosho 638,000 kwa ajili ya kuwapatia miche hiyo bure wakulima wake wanaozalisha zao hilo katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Afisa kilimo wa halmashauri hiyo, Chiza Malando alisema miche hiyo imezalishwa kupitia vikundi vya wakulima ambavyo vilipatiwa elimu juu ya uzalishaji huo na mwitikio wake katika utekelezaji wa jambo hilo umekuwa mzuri. Lengo la kufanya hivyo ni kuweza kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo ni tegemeo kubwa kwa kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo. Malando alisema, mpango huo ulianza tangu mwaka 2008 kupitia sekta ya  uendelezaji wa kilimo nchini, hata hivyo bado kulikuwa na mwamko mdogo am
VYAMA TISA KUPAMBANA UCHAGUZI NAFASI YA UBUNGE SONGEA

VYAMA TISA KUPAMBANA UCHAGUZI NAFASI YA UBUNGE SONGEA

News Bulletin
VYAMA tisa vimejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Tina Sekambo amevitaja vyama ambavyo hadi sasa tayari vimekwisha jitokeza kuchukua fomu hizo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), UPDP, Demokrasia Makini, AFP, TLP, CCK, NRA, ADA na TADEA. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hadi kufikia jana bado hakikujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi huo, ambao unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Leonidas Gama wa CCM kufariki dunia mapema mwezi uliopita. Pia Sekambo alieleza kuwa mwisho wa kuchukua  na kurudisha fomu hizo ilikuwa ni Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 10  huku akisisitiza kuwa Ofisi yake haitak
Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.  Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake.

Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake.

News Bulletin
Kiongozi mpya wa chama cha ANC cha Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amefunga rasmi mkutano wa chama hicho akiahidi kufanyia kazi sera za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. Akizungumza katika kikao kilichomalizika usiku wa manane, Ramaphosa amesema kupambana na rushwa sambamba na umaskini ni kipaumbele cha kwanza kwa chama chake. Ramaphosa na Zuma awali walikua marafiki wa karibu Amesema kuwa kikao cha kamati kuu kimeahisi pia kurudisha ardhi muhimu ambazo zilikua mikononi mwa wasiohitajika ikiwa ni lengo la kukuza sekta ya kilimo. Amemsifu mpinzani wake wa kaziribu ayembwaga kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa ANC Nkosazana Dlamini Zuma kuwa ni jasiri na mchapa kazi. CHANZO: BBC
Yaliyojiri Katika Ziara ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mkoa wa Kaskazini Pemba

Yaliyojiri Katika Ziara ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Mkoa wa Kaskazini Pemba

News Bulletin
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Bwana Omari Khamis Othman Akizungumza na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu (kulia) na Ujumbe aliofuatana nao alipomtembelea ofisini kwake, wakati akiendelea na ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 – 21 Disemba, 2017. Mkuu huyo wa Mkoa aliahidi kushughulikia kwa karibu ombi lilitolewa na Kamishna Sururu, la kupatiwa Viwanja kwenye maeneo yaaliyotengwa na Serikali ili kujenga Nyumba za Makaazi ya Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani humo.  Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akisikiliza maelezo yanayotolewa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Iddi A. Iddi wa Kituo cha Uhamiaji Bandari ya Wete, kuhusu ukaguzi wa Watu wanaotumia Bandari hiyo, ambapo vyombo vyake havijaruhusiwa kisheria kusafirisha abiria. Ilielezwa kuwa hiyo ni changamo
error: Content is protected !!