
SIMULIZI YA MWANAMKE: MKE WA PILI
AS SALAM A'LAYKUM,
Mke wa pili! Ni maneno yaliyorindima na kutoa mwangwi katika kichwa changu.
Nilimuuliza: Kwa nini? Je mie sio mrembo? Abadan! Kamwe sitakubali suala la mke wa pili. Kama unataka mke wa pili waweza kwenda kumchukua lakini utambue kuwa ukirudi hutanikuta hapa!”
Hayo yalikuwa ni maneno yangu niliyomwambia mume wangu miaka kadhaa iliyopita aliponitamkia kuwa anakusudia kuoa mke wa pili.
Alinieleza kuwa ni mwanamke ambaye alikuwa ameachika muda si mrefu na alikuwa na watoto 4 na Yuko katika wakati mgumu na hajui mahali anapoweza kupata chakula au hana uhakika wa kuwahudumia wanaye.
Baba yao yu wapi? Nilimuliza. Huyo baba hawezi kuwatunza wanaye? Kwa nini wewe mtu wa mbali ubebe mzigo wa mwanaume mwingine? Kuna njia nyingine za kumsaidia kiuchumi bila kulazi...