Tanzania yatangaza siku nne za maombolezo

Tanzania yatangaza siku nne za maombolezo

Jamii, Mikoani
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ametangaza siku 4 za maombolezo kuanzia Ijumaa kufuatia ajali ya Ferri ya MV Nyerere kuzama katika ziwa Victoria siku ya Alhamisi. Katika ajali hiyo watu zaidi ya 130 wamethibitishwa kupoteza maisha kufikia Ijumaa, huku wengine zaidi ya 40 wakiwa tayari wamesha okolewa. Serikali imesema zoezi hilo la uokoaji linaendelea. Taarifa za awali zinaeleza kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba mizigo na abiria wengi zaidi ya uwezo wa Ferri hiyo. Serikali tayari imetuma wachunguzi katika eneo la tukio la ajali hiyo kufanya uchunguzi wa kina. Rais Magufuli ameagiza watendaji wa Kivuko na wengine wote wakamatwe katika hali ya uchunguzi huo, akiwemo kapteni wa meli hiyo. Shirika la habari la Reuters liliwanukuu maafisa wa serikali ya Tanzania waki...
Mapigano yashtadi Libya, waliouawa Tripoli wapindukia 96

Mapigano yashtadi Libya, waliouawa Tripoli wapindukia 96

Kimataifa
Wizara ya Afya nchini Libya imetoa indhari juu ya kushadidi mapigano katika mji mkuu Tripoli, ambapo idadi ya waliouawa katika ghasia hizo imeongezeka na kufikia watu 96, wakiwemo raia. Vyombo vya dola leo Ijumaa vimeripoti kuwa, mbali na watu 96 kuuawa katika mapigano hayo kufikia sasa, wengine 16 hawajulikani waliko huku 444 wakijeruhiwa. Taarira ya Wizara ya Afya ya Libya imebainisha kuwa, familia 123 zimelazimika kuyahama makazi yao kutokana na kushtadi mapigano hayo yaliyoanza tangu Agosti 26. Jana Alkhamisi pekee, watu 11 wakiwemo raia wanane waliuawa huku wengine 33 wakijeruhiwa kusini mwa mji mkuu Tripoli. Ghassan Salamé, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa makundi yanayovunja makubaliano ya kusitisha vita nchini humo yatawekewa vik
Dkt. Shein aweka mawe ya msingi skuli 9 za ghorofa Unguja na Pemba

Dkt. Shein aweka mawe ya msingi skuli 9 za ghorofa Unguja na Pemba

Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa azma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kutangaza elimu bure kwa watoto wa Zanzibar bila ubaguzi ilikuwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha ASP ambayo inaendelea kutekelezwa hadi hivi leo. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla ya uwekaji mawe ya Msingi ya Skuli 9 za ghorofa Unguja na Pemba ambapo kwa niaba ya skuli hizo aliweka jiwe la msingi skuli ya Kinuni, Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni kati ya skuli hizo mpya hatua ambayo ni miongoni mwa shamrashamra za kusherehekea miaka 54 ya Elimu bure ambapo kilele chake ni Septemba 23 mwaka huu. Rais Dk. Shein alisema kuwa utekelezaji huo unaendelea kutoka kwa chama cha ASP na hivi sasa CCM ambapo ujenzi wa skuli hizo ni ute...
TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.

TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.

Biashara & Uchumi, Mikoani
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao. Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao. Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini mada kuh
Uturuki itaendelea na mapambano dhidi ya ugaidi nchini Syria

Uturuki itaendelea na mapambano dhidi ya ugaidi nchini Syria

Kimataifa
Uturuki yafahamisha kuwa  jeshi lake litaendelea kupambana na  ugaidi nchini Syria na kutolea wito jumuiya ya kimataifa kuwajibika ipasavyo. Taarifa iliotolewa  na baraza la usalama la Uturuki baada ya mkutano wake uliofanyika Alkhamis mjini Ankara imefahamisha kuwa jeshi la Uturuki katika  mapambano yake dhidi ya ugaidi litaendelea na operesheni zake nchini Syria. Katika mkutano huo kulizungumziwa pia kuhusu mapambano dhidi ya makundi yote ya kigaidi yanayojaribu kuendelea kuyumbisha usalama katika ukanda, makundi hayo ni kundi la wahaini wa FETÖ, kundi la PKK na tawi la YPG na kundi la wanamgambo wa Daesh. Magaidi wanaokamatwa na jeshi la Uturuki katika operesheni   zake watahukumiwa nchini Uturuki. Hatua hiyo ambayo imechukuliwa na Uturuki ni ishara kuwa imedhamiria ku
error: Content is protected !!