Oman Air Yakabidhi Tiketi Kwa Washindi wa Bahati Nasibu ya Kuchangia Damu Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Mkuu wa mkoa wa mjini magharib unguja Mhe, Ayoub muhaamed mahmod kushirikiana na shirika la ndege la Oman Air wamekabidhi tiketi tatu za kusafiri kwa washindi wa droo ya bahati nasibu ya kuchangia damu iliyofanyika katika bonanza la uchangijaji wa damu katika mkoa wa mjini
magharib unguja ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki hii.

Washindi hao watatu Mohamed mussa Ayoub mkaaz wa chumbuni ,Abdallah Alaw mkazi wa kwerekwe na Maulia Mwinyi mzee ambaye ni diwani wa Mombasa walipatikana mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo iliyokuwa na watu 543 waliojitokeza kuchangia damu kwa hiari katika bonanza la uchangiaji wa damu salama kisonge mkoa wa mjini unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo maalum ya kuwakabidhi tiketi za kusafiri kwa washindi wa droo hiyo mkuu wa mkoa wa mjini magharib mhe, Ayoub Mohammed Mahmud amewapongeza washindi hao kwa kufanikiwa kushinda nafasi hiyo ya kuweza kwenda kutembea katika mji mmoja kati ya mji wa Dubai,Oman , Bangkok na Bombay kwa siku mbili huku gharama za safari ya kwenda kurudi ikigharimiwa na Oman air huku huduma za malazi na makazi ziki gharamiwa na ofisi ya mkoa wa mjini magharib unguja.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

CHANZO: ZANZINEWS

 

error: Content is protected !!