Tuesday, September 28
Shadow

News Release

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi Agosti 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi Agosti 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.

Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 25, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania. Mhe. Rais awali alikutana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mubarak Mohammed Alsehaijan. Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar pamoja na kuipatia Zanzibar misaada mbalimbali katika sekta za kijamii. Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Dk. Mwinyi alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda, Meja Jenerali Charles Karamba. Katika mazungumzo hayo Balozi Karamba alimueleza Mhe Rais mpango wa Shirika la Ndege la Rwanda ‘Air Rwanda’ kuanza safari zake kati ya Kigali na Zanzibar ifikiapo katikati ya mwaka 2022, hatua ambay...
Sitholizwe Mdlalose appointed as Managing Director of Vodacom Tanzania Plc

Sitholizwe Mdlalose appointed as Managing Director of Vodacom Tanzania Plc

Vodacom Tanzania Plc Chairman of the Board of Directors, Judge (Rtd) Thomas B. Mihayo is pleased to announce the appointment of Sitholizwe Mdlalose as the new Managing Director. Sitholizwe joins the company from Vodacom South Africa (VSA) where he was the Finance Director since 2017. Sitholizwe has previously  held various roles in the Vodacom Group including that of Interim Chief Finance Officer as well as Chief Finance Officer of Vodacom Group’s International Business. Prior to joining Vodacom Group, he worked with Vodafone Group for more than 6 years holding senior roles within the Group. He has more than 19 years of finance, management and consulting experience, of which 13 have been in telecommunications across both emerging and developed markets. He holds a Bachelors of Accounting...
Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji

Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji

RAIS wa Zanzibar ambae pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji.Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo leo Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana na Balozi Mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar Agostino Abacar Trinta aliefika Ikulu kujitambulisha. Amesema nchi hizo zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu, hali inayotoa fursa kwa Wazanzibari wengi kupata fursa ya kuishi na kufanyakazi mbali mbali nchini humo, hususan eneo al Kaskazini mwa nchi hiyo.Aidha, alisema nchi hizo zimekuwa zikiunganishwa kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Rais wa nchi hiyo Felipe Nyusi ndie Mwenyekiti wake Nae, Balozi Mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar A...
Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Pemba yaunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi ya Shaibu Foundation

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Pemba yaunga mkono juhudi zinazofanywa na taasisi ya Shaibu Foundation

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Pemba imeiunga mkono taasisi ya Shaibu Foundation kwa kuiruhusu taasisi hiyo kutumia vituo vyake vya TEHAMA-JAMII kwa lengo la kusaidia kufanikisha mradi wake ujulikanao kama  “e-Learning for Primary & Secondary Schools’ Project – Phase Two”   Akikabidhi barua ya udhibitisho wa kukubali taasisi hiyo kutumia vituo hivyo katika ufundishaji Ahmed B. Said kwa niaba ya Ofisa mdhamini amesema wizara haina pingamizi juu ya matumizi ya vituo hivyo vya Tehama kwa kuwafundisha walimu kwani itasaidia kukuza taaluma kwa walimu hao na kuwa na weledi zaidi katika ufundishaji. Vituo hivyo vitatumika kwa skuli zilizo karibu na ambao hawana vifaa vya Tehama au Chumba cha Computer kwenye skuli husika.   Akieleza Lengo kuu hasa la mafunzo hayo Rais wa Shaib...
Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba maendeleo na ibada haviwezi kufanyika iwapo hapatakuwa na amani

Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba maendeleo na ibada haviwezi kufanyika iwapo hapatakuwa na amani

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba maendeleo na ibada haviwezi kufanyika iwapo hapatakuwa na amani.Alhaj Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa salamu zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wote mara baada ya Sala ya Ijumaa huko katika Msikiti wa Wireless, Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi. Katika salamu hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kuwa amani ni ajenda ya kudumu, hivyo, kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha amani inadumishwa hapa nchini.Alhaj Dk. Mwinyi alisisitiza kwamba jamii yote ina wajibu ya kuidumisha amani huku akieleza kwamba katika kuimarisha na kudumisha amani lazima misukusuko itakuwepo lakini ni vyema jamii inapiga hatua na inavuka. Alisema kwamba hakuna ja...