Ndege ya jeshi la Marekani yafanya ajali katika kisiwa cha Japan

Ndege ya jeshi la Marekani yafanya ajali katika kisiwa cha Japan

Ndege ya jeshi la Marekani imefanya ajali ikiwa na watu 11 katika kisiwa cha Japani cha Okinawa katika bahari ya Pasifiki.

Waziri wa ulinzi wa Japani Itsunori Onodera amefahamisha kuwa wafanyaki wanane wa ndege hiyo wamepatikana wakiwa salama.

Wafanyakazi wengine watatu bado wanatafutwa.

Ndege hiyo iliofanya ajali ni aina ya C2 na ilipata ajali ikiwa katika umbali wa kilomita 150 Kaskazini-Magharibi mwa Okinotori-shima Kusini mwa Japan.

 

error: Content is protected !!