Mamilioni yalipotea katika mazishi ya Mandela

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

MAZISHI  ya aliyekuwa rais wa zamani Afrika kusini ,Nelson Mandela yanadaiwa kukumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.

Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imebaini kuwa takriban dola millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka nne ilyopita.

Ripoti hiyo ilisema kwamba viongozi hao walivuja pesa na kukiuka taratibu zilizowekwa huku ikisemekana kwamba gharama za bidhaa ziliongezwa maradufu na matumizi mazishi kutajwa kuwa ya juu sana kwa mfano shati za kumbukumbu ya mazishi zilinunuliwa kwa dola  25 badala ya dola 19 .

Hata hivyo ripoti hiyo imetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliofanya jambo hilo la kushangaza katika jamii.

CHANZO: BBC

error: Content is protected !!