Sunday, July 3
Shadow

MABADILIKO YA TAREHE YA SHEREHE YA KUWAZAWADIA WALIMU

SFL/E/2021/TO/08112021SF04

November 08, 2021 G                                                                                                            02 Rabi-Al-Thani, 1443 H

Taarifa kwa umma,

MABADILIKO YA TAREHE YA SHEREHE YA KUWAZAWADIA WALIMU

Salamu kutoka Shaibu Foundation,

Kwa kupitia barua hii tunautaarifu umma kwamba tarehe ya sherehe tuliotarajia kuifanya ya kuwakabidhi vyeti walimu walioshiriki mafunzo ya elimu mtandao kwa skuli za msingi na sekondari – awamu ya pili imebadilika kutoka tarehe 14/11/2021 na kusogezwa mbele hadi tarehe 05/12/2021.

Sababu kuu ni kutokana ratiba za mitihani ya wanafunzi inayoendelea na inayotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.

Shaibu Foundation tukiwa mdau mkubwa wa elimu tumeonelea ni vyema tukaisogeza mbele shughuli yetu hii.

Angalizo, kilichobadilika ni tarehe ya shughuli tu, mambo  mengine yote yako vile vile. Na kuhusu sehemu/ukumbi itakapofanyika, muda na mambo yote yanayohusiana na shughuli yetu hii tutawapatia taarifa zaidi muda ukikaribia In Shaa Allah.

Wako mdau wa elimu, kwa pamoja tunaboresha elimu kidijitali,

 

Imetolewa  na

Uongozi wa taasisi ya shaibu foundation