Sunday, July 3
Shadow

Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji

RAIS wa Zanzibar ambae pia Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji.Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo leo Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana na Balozi Mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar Agostino Abacar Trinta aliefika Ikulu kujitambulisha.

Amesema nchi hizo zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu, hali inayotoa fursa kwa Wazanzibari wengi kupata fursa ya kuishi na kufanyakazi mbali mbali nchini humo, hususan eneo al Kaskazini mwa nchi hiyo.Aidha, alisema nchi hizo zimekuwa zikiunganishwa kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Rais wa nchi hiyo Felipe Nyusi ndie Mwenyekiti wake

Nae, Balozi Mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar Agostino Abacar Trinta, aliipongeza Zanzibar kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizo, kwa maslahi ya wananchi wa pande mbili pamoja na misaada mbali mbali inayotoa kwa nchi yake.Balozi Trinta amemtakia afya nje na maisha marefu Rais wa Zanzibar na Mwenyektii wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, yeye pamoja na familia yake.Aidha, Balozi huyo alitumia fursa hiyo kuwasilisha barua maalum ya salamu kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na barua ya Utambulisho.

 

CHANZO: TOVUTI YA IKULU