Listing Details

Report Abuse

mufti_logo-150×150

Ofisi ya Mufti wa Zanzibar (The Mufti’s Office of Zanzibar)

Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 1992 kwa Amri ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa wakati huo Mhe. Dk.Salmin Amour Juma. Aidha, baadae ikaanzishwa upya kwa Sheria ya Mufti Namb. 9 ya mwaka 2001. Kabla ya kuanzishwa  Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar baadhi ya kazi  za msingi zilikuwa zikifanywa na Mashekhe mbali mbali wakiwemo wale wa Msikiti Gofu, wakiwemo Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Fatawi bin Issa n.k ambao walikuwa wakitoa Fatwa mbali mbali, utatuzi wa migogoro na kutoa Miongozo mbali mbali kwa kadri ilivyohitajika kwa wakati huo.  Ama kwa upande wa Serikali, Mahkama ya Kadhi Mkuu ilikuwa ikitumika kwa madhumuni hayo.

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنْتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُمْ بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنْتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِفَأَنْقَذَكُمْ مِنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُون

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. “Qur-an 4:103”

Ofisi ya Mufti inatoa huduma kwa jamii, huduma zinazotolewa ni Usajili wa Misikiti, Madrasa, Kusilimisha wasiokua waislamu, Kuendesha mafunzo ya ndoa, kutoa fatwa katika mambo mbalimbali ya kiislamu na kusuluhisha migogogoro ya ndoa.

Utaratibu wa Usajili wa Misikiti/Madrasa

Kabla ya kufika Ofisi ya Mufti, muhusika anatakiwa kwanza aandike barua yake yenye kichwa cha habari ya ombi la kusajili Msikiti/Madrsa.

Katika barua hiyo anatakiwa aeleze habari zote muhimu zinazo jitosheleza na ombi lake la Msikiti/Madrasa

USAJILI WA MISIKITI

Katika ombi la usajili wa Misikiti Mteja anatakiwa  ataje jina la msikiti wake, pahala ulipo, Shehia, Wilaya na Mkoa. Aeleze mwaka uliojengwa Msikiti, waliojenga msikiti kamani Mfadhili au waumini wenyewe. Ainishe kama msikiti unasaliwa Ijumaa au hausaliwi Ijumaa.

Pia aeleze wastani wa watu wanao Sali katiak Msikiti huo, na sehemu  ya kusalia wanawake imo au haimo katika msikiti.

Na mwisho utajwe uongozi wa Msikiti kwa majina yao pamoja na namba zao za simu kama ifuatavyo:-

  1. Imamu Mkuu
  2. Msaidizi Imamu
  3. Muadhini
  4. Katibu na
  5. Mshika Fedha

Barua hii ya ombi la usajili wa Msikiti ipitie kwa Sheha wa Shehia uliopo Msikiti huo na Sheha atoe barua ya ombi la usajili wa Msikiti yenye anuani ifuatayo.

Katibu wa Mufti,

Ofisi ya Mufti

P.O.Box 2479

Zanzibar.

Barua zote mbili ziletwe ofisi ya Mufti kwa kuomba kusajili Msikiti.

USAJILI WA MADRASA

Katika kusajili madrasa unafuata utaratibu kama ulioelezwa katika usajili wa  misikiti ispokua usajili wa Madrasa utaengeza mambo ya fuatayo.

  • Barua hii itaje idadi ya wanafunzi wote, idadi ya wanafunzi wanawake na wanaume.
  • Barua itaje masomo yote yanayo someshwa katika Madrasa hiyo, na inapendekezwa masomo yasipungue saba.
  • Barua iainishe uongozi wachuo pamoja na namba zao za simu.

Hatua au jinsi ya utaratibu wa Kusilimisha wasiokuwa Waisilamu

Zinatolewa huduma kwa walio silimu na wale wanaotaka kusilimu bure. Huduma hii ni ambayo haicheleshwi hata kidogo. Ndani ya nusu saa mwenye kusilimu anakabidhiwa tarjisi yake ya kusilimu.

Utoaji na Uendeshaji wa Mafunzo ya Ndoa

Kwa vile ofisi ya Mufti imejipanga vizuri sana. Masomo ya ndoa yanatolewa bure ndani ya muda wa meizi miwili na nusu kwa siku za Jumamosi na Jumapili tu, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa sita mchana.

Fomu za mafunzo ya ndoa zinapatikana Ofisi ya Mufti bure, muhusika atajaza fomu ya mafunzo ya ndoa na kuirejesha ofisini. Na baada ya masomo vyeti vya uhitimu vinatolewa bure, ambavyo thamani yake  ni kubwa mno katika jamii

Contact Information

Author Info

Administrator

Member since 2 years ago
View Profile

0 Reviews

You need to Login or Sign Up to submit a review

Save on your hotel - hotelscombined.com