Daraa Yakombolewa, Jeshi la Syria Lakaribia Kudhibiti Kikamilifu Eneo la Kusini

Daraa Yakombolewa, Jeshi la Syria Lakaribia Kudhibiti Kikamilifu Eneo la Kusini

Jeshi la Syria limetangaza kwamba mji wa Daraa ulioko kusini mwa nchi hiyo umekombolewa kikamilifu.

Ukombozi wa mji wa Daraa una umuhimu mkubwa wa kistratijia. Moja kati ya sababu za umuhimu huo wa kistratijia ni kwamba mji huo ndiko ilikoanzia cheche ya kwanza ya¬†malalamiko ya ndani nchini Syria ambayo baadaye yalitumiwa vibaya na madola ya kibeberu na kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vya zaidi ya miaka saba sasa. Kwa sababu hiyo pia mji wa Daraa unatajwa kuwa susu na “chimbuko la mapinduzi” ya Syria. Maeneo mengi ya Daraa yamekuwa yakidhibitiwa na makundi ya kigaidi katika kipindi chote cha miaka 7 iliyopita.

Sababu ya pili inayozidisha umuhimu wa kistratijia wa kukombolewa mji wa Daraa ni nafasi yake muhimu ya kijiografia. Daraa iko karibu na mpaka wa Syria na Jordan na Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Kwa msingi huo imekuwa ikitumiwa kama njia salama ya kuingiza magaidi wa Kiwahabi nchini Syria kutokea Jordan. Wakati huo huo utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zimekuwa zikiishinikiza serikali ya¬†Syria kupitia njia ya kuyasaidia kwa hali na mali makundi ya kigaidi na ya waasi katika mkoa wa Daraa. Kukombolewa mji huo kunainyang’anya Marekani na mwanaharamu wake, Israel silaha hiyo muhimu.

Jeshi la Syria baada ya kukomboa mji wa Daraa

Kuhusu umuhimu wa kijiografia wa Daraa, jarida la kila wiki la al Us’buu la Misri limeandika kuwa: Ukombozi wa Daraa una umuhimu mkubwa hata zaidi ya kukombolewa maeneo mengine ya Syria, kwani serikali ya Damascus ilikuwa na habari kamili kuhusu njama na mipango ya kutaka kuigawa nchi hiyo. Kwa mujibu wa njama hiyo, ilipangwa kuwa, ili kuweza kudhamini suala la kukaliwa kwa mabavu eneo la Haudhul Yarmuk, na kutwaliwa kikamilifu na daima miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na Israel, eneo la Daraa pia linapaswa kuunganishwa na maeneo hayo.”

Nukta nyingine kuhusu umuhimu wa kukombolewa Daraa ni kwamba ukombozi wa eneo hilo utarahisisha ukombozi wa maeneo mengine kama mkoa wa Quneitra. Vilevile wapinzani wa serikali ya Syria wamekuwa wakitumia Daraa kwa ajili ya kupitisha magaidi na kuwaingiza nchini humo lakini sasa njia hiyo imefungwa baada ya kukombolewa eneo hilo. Katika upande mwingine mkoa wa Quneitra wenye idadi kubwa sana ya magaidi wanaoungwa mkono na nchi za kigeni, uko magharibi mwa Daraa; hivyo kukombolewa mji huo kutaliwezesha jeshi la Syria na waitifaki wake kukomboa pia mkoa wa Quneitra.

Jeshi la Syria

Suala jingine ni kwamba, kukombolewa Daraa ni hatua nyingine muhimu katika njia ya kukomeshwa vita nchini Syria na kufungua ukurasa mpya wa utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo. Mchambuzi Ali al Ghallaf ameandika katika mtandao wa al Akhabari kwamba: Kukombolewa mji wa Daraa kuna maana ya kufungwa ukurasa ya matumizi ya njia za kijeshi na kunawavunja matumaini wale wote waliodhani kwamba, Damascus itatekwa na kuchukuliwa na wapinzani wa Bashar Assad kupitilia lango la kusini mwa Syria. Hali ya Daraa na kusini kwa ujumla ni bishara njema ya kumalizika vita nchini Syria.”

Inatupasa pia kusema kuwa, hatua ya jeshi la Syria ya kukomboa Daraa na kulidhibiti eneo hilo inatambuliwa kuwa ni kufeli mpango wa Marekani, Saudi Arabia, utawala wa Kizayuni wa Israel na washirika wao wa kutaka kuunda jimbo au kijiinchi kingine kinachojumuisha maeneo ya Daraa, Quneitra na Suwayda huko kusini mwa nchi hiyo. Hivyo basi, baada ya mafanikio hayo makubwa katika medani ya vita, serikali ya Syria imepata turufu muhimu sana inayoweza kutumiwa vyema katika meza ya mazungumzo ya kisiasa.

error: Content is protected !!