Thursday, October 6
Shadow

Updates

Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Misikiti pamoja na Madrasa zinazojengwa zinapaswa kutumika kuielimisha jamii umuhimu wa malezi bora ya watoto ili wawe na khofu ya Mungu.

Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Misikiti pamoja na Madrasa zinazojengwa zinapaswa kutumika kuielimisha jamii umuhimu wa malezi bora ya watoto ili wawe na khofu ya Mungu.

RAIS wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Misikiti pamoja na Madrasa zinazojengwa zinapaswa kutumika kuielimisha jamii umuhimu wa malezi bora ya watoto ili wawe na khofu ya Mungu.Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo, katika ufunguzi wa Msikiti mpya wa Al hudda uliopo eneo la Masingini Wilaya Magharibi ‘A’ Unguja, uliojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya ‘Al-noor Cheritabla Agency for the Needy’, hafla iliokwenda sambamba na Ibada ya Sala ya Ijumaa. Amesema kumekuwepo mmong’onyoko mkubwa wa maadili katika jamii hususan kwa vijana kujihusisha na vitendo viovu, ikiwemo vya Udhalilishaji, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na Wizi na ubadhirifu wa mali za Serikali, mambo aliyoeleza yanapaswa kuzungumzwa na kupatiwa ufumbuzi kupitia Misiki...
Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali itatoa tamko kuifanya siku ya mwaka mpya wa kiislamu kuwa ya mapumziko

Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali itatoa tamko kuifanya siku ya mwaka mpya wa kiislamu kuwa ya mapumziko

Rais wa Zanzibar ambae pia ni  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali itatoa tamko kuifanya siku ya mwaka mpya wa kiislamu kuwa ya mapumziko.Alhaj D. Mwinyi aliyasema hayo jana katika kongamano la maadhimisho ya mwaka mpya wa kiislamu 1444, lililofanyika msikiti wa Jamiu Zinjibar, Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi. Aidha alisema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika kwa mzunguko kati ya Unguja na Pemba ili kutoa nafasi kwa Waislamu kushiriki. Aliipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuandaa maadhimisho hayo ambayo ni utaratibu mpya kufanyika visiwani hapa na inatoa fursa kwa waislamu kujua mwaka wao kwa mujibu wa tahehe za dini yao. “Hakuna asieujua mwaka mpya ule wa kawaida na siku ya mwaka mpya ikifika basi kila mtu anajua lak...