Sports

SERENA, VENUS NDANI YA NUSU FAINALI FED CUP

SERENA, VENUS NDANI YA NUSU FAINALI FED CUP

Sports
CAROLINA, Hispania SERENA na Venus Williams wamechaguliwa katika timu ya tenisi ya Marekani kukabiliana na Ufaransa katika nusu fainali za Fed Cup, Shirika la Tenisi la Marekani (USTA) limetangaza. Madada hao walicheza katika mechi ya kwanza ya Uholanzi huko North Carolina mwezi Februari na kufanikiwa kutinga nusu fainali hiyo itakayochezwa katika mji wa Aix-En nchini Ufaransa Aprili 21 na 22 mwaka huu. Mchezo mwengine wa nusu fainali utakuwa kati ya timu ya Ujerumani dhidi ya Jamhuri ya Czech utakaochezwa mjini Stuttgart.
Real Madrid yaingia nusu fainali Ligi ya Washindi baada ya kuichabanga Juve

Real Madrid yaingia nusu fainali Ligi ya Washindi baada ya kuichabanga Juve

Sports
Timu ya Real Madrid  yatinga nusu fainali baada ya kuilaza timu ya Juventus kwa mabao lililosawazishwa na Cristiano Ronaldo. Timu ya Real Madrid yaichapa timu ya Juventus  kutoka Italia katika uga wa Santiago Bernabeu katika mechi ilichezwa Jumatano kati ya mahasimu hao. Real Madrid imechapa mabao matatu kwa nunge timu ya Juve na kuipa tikiti ya kuingia katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Washindi ya Ulaya. Goli la mkwaju wa panati lililosawazishwa na Cristiano Ronaldo katika dakika za mwisho limeiingiza timu ya Real Madrid katika nusu fainali ya michuano ya Ligi kuu ya washindi ya Ulaya. Penati hiyo iliamliwa na muongoza mchezo baada y aya Medhi Benatia  kumdodosha Lukas Vazquez  katika eneo la hatari .
Shaba FC : kifuatacho sasa ni kichapo tu kwenda mbele

Shaba FC : kifuatacho sasa ni kichapo tu kwenda mbele

Local, Sports
PICHA KUTOKA MAKTABA MTANDAO: Beki wa timu ya Shaba Hassan Suleiman, akikimbilia mpira huku mchezaji wa timu ya Mtende Rangers, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt. Imeandikwa na Salim Hamad , Pemba BAADA ya Kufanya vyema Klabu ya Shaba FC katika mchezo dhidi ya FSC , hatimae nahodha wa timu hiyo Abdalla Salum Abdall ametamba kuwa  sasa ni mwendo wa kutoa dozi tu kwenye michezo inayosalia ili kuhakikisha inatinga hatua ya Nane bora na hata kutwaa ubingwa msimu huu. Shaba ilitoa kichapo  cha mabo 2-1 FSC katika mfululizo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba, mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani Visiwani hapa. Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kumalizika kwa mchezo  huo Nahodha huyo alisema kiu yao ni kuona timu yao inaingia kwenye hatua ya Nane bora itakashiriki
TIMU ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) imepangwa katika kundi la kifo kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018.

TIMU ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) imepangwa katika kundi la kifo kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018.

Sports
TIMU ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) imepangwa katika kundi la kifo kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018. Habari zilizopatikana na Mtandao huu kutoka kwa CECAFA zinaeleza kuwa Zanzibar imepangwa kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na baraza hilo inaonesha kuwa Zanzibar itaanza kampeni za kutwaa taji hilo, kwa kucheza na Sudan April 15 katika uwanja wa Gitega majira ya saa 7:30 za mchana. Tayari Zanzibar imechagua wachezaji 20 na ipo katika maandalizi makali chini ya kocha mkuu Mzee Ali Abdallah, ambapo Vijana hao wapo kambi katika Hoteli ya Zanzibar Paradise International iliyopo Uwanja wa Amaan. Katika
Mambo motomoto uwanja wa Gombani Pemba.

Mambo motomoto uwanja wa Gombani Pemba.

Local, Sports
  WACHEZAJI wa Timu ya ZECO wakisalimiana na wachezaji wa ZAWA wakati wa mchezo wa Mei Mosi yaliyoanza kutimua vumb I lake katika uwanja wa michezo Gombani, ZECO kuibuka na ushindi wa bao 4-1.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) MKUFUNZI wa waamuzi Kisiwani Pemba na mwamuzi wa FIFA mstaafu Ali Juma Salim katikati, akiwa katika picha ya Pamoja na waamuzi chipkizi wanaochezaji ligi za madaraja mbali mbali Kisiwani hapa, kabla ya kuanza kwa mashindano ya Mei mosi ambapo ZECO iliibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya ZAWA.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA). MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akisalimiana na wachezaji wa timu ya ZAWA, kabla ya kufungua rasmi mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika uwanja wa Gombani, ZECO kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya ...
error: Content is protected !!