Regional

WAKALA WA MAJENGO TBA IMEKABIDHI MABWENI MATATU NA MADARASA MAWILI YA WASIOONA SONGEA

WAKALA WA MAJENGO TBA IMEKABIDHI MABWENI MATATU NA MADARASA MAWILI YA WASIOONA SONGEA

Regional
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili ya shule ya msingi Luhira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo na Manispaa ya Songea, Meneja wa TBA Mkoa wa Ruvuma Edwin Nunduma amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa mabweni matatu na ukarabati wa madarasa mawili kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 151 Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TBA kila bweni Lina uwezo wa kulaza wanafunzi 12 hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi wenye ulemavu 36. Mkuu wa shule hiyo Joyce Konga ameishukuru serikali kwa kuwajengea mabweni ya kisasa na kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu,  amesema shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 48 wenye ulemavu n
Rais Dkt. Magufuli azindua rasmi taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)

Rais Dkt. Magufuli azindua rasmi taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)

Regional
Msanii anayechipukia  Goodluck Gozbert akitumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa "Hauwezi Kushindana" kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza msanii anayechipukia  Goodluck Gozbert baada ya kutumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa "Hauwezi Kushindana" kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018  Mshauri mwelekezi wa JMKF Bi. Aisha Sykes akiwa na mwezeshaji Aidan Eyakuze wakifanya mawasilisho ya mpango mkakati wa tasisi hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA SONGEA KUTEMBELEA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA KATA YA TANGA MANISPAA YA SONGEA

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA SONGEA KUTEMBELEA UJENZI WA MACHINJIO YA KISASA KATA YA TANGA MANISPAA YA SONGEA

Regional
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea MRADI wa machinjio ya kisasa unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu unaotarajia kukamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu. Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Songea katika kukagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa inayojengwa kata ya Tanga manispaa ya Songea. Mradi huo unaojengwa katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea kwa sasa umefikia asilimia 80 ya ujenzi wake, Mkandarasi wa ujenzi ujenzi huo Kampuni ya Giraffe ameahidi kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo kabla ya tarehe ya mwisho wa mkataba ambapo mkataba wa ujenzi ulianza Julai 2017 na kukamilika Julai 2018. Manispaa ya Songea imekuwa ikij...
BUSTANI MANISPAA SONGEA KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO

BUSTANI MANISPAA SONGEA KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO

Business, Regional
Mandhari ya bustani ya Manispaa Songea Mkoani Ruvuma. Na Kassian Nyandindi,      Songea. MRADI wa bustani ya Manispaa ya Songea uliopo Mkoani Ruvuma, umekamilika na kwamba unatarajia kuanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, ambapo Mkandarasi husika tayari amekabidhi mradi huo kwa uongozi wa Manispaa hiyo. Kaimu Mkuu wa idara ya ujenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Nicolous Danda alisema kuwa mradi huo ulikamilika tangu mwezi Desemba mwaka 2017 huku Mkandarasi aliyepewa jukumu la ujenzi wa bustani hiyo akipewa matazamio ya miezi sita ya ujenzi wa mradi huo ambayo inaishia mwezi Aprili mwaka huu. Danda amezitaja kazi zilizosalia katika mradi huo kuwa ni kuendelea kuotesha nyasi, kufunga mfumo wa maji taka ambayo inafanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (SOUWASA)
WACHINA WAANZA UJENZI STENDI MPYA MANISPAA SONGEA

WACHINA WAANZA UJENZI STENDI MPYA MANISPAA SONGEA

Business, Regional
Wataalamu wa Kampuni ya kichini ya SIETCO wakiwa pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Songea, katika eneo la ujenzi wa Stendi mpya ya mabasi ya abiria ambayo ujenzi wake tayari umekwisha anza.  Na Kassian Nyandindi,    Songea. HATIMAYE Kampuni ya Serikali kutoka nchi ya China inayofahamika kwa jina la, China Sichuan International Cooperation (SIETCO) imewasili mjini Songea tayari kwa kuanza kazi ya ujenzi wa Stendi mpya ya kisasa kwa ajili ya magari ya abiria, katika eneo la Kata ya Tanga Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. SIETCO imesaini mkataba wa miezi 18 kwa ajili ya kazi ya ujenzi huo na Halmashauri ya Manispaa hiyo, kujenga Stendi mpya ya mabasi katika eneo hilo la Tanga kuanzia Aprili Mosi mwaka huu. Mwakilishi wa Kampuni hiyo ameiambia Kamati ya ulinzi n
error: Content is protected !!