Nyumbani

Wapingaji baa mjini waingia mitini

Wapingaji baa mjini waingia mitini

Biashara & Uchumi, Jamii, Nyumbani
MAHAKAMA ya vileo Zanzibar, imeelezea kusikitishwa na wananchi wa wilaya ya mjini kutofika mahakama ya Mwanakwerekwe, kupinga baa zilizomo ndani ya wilaya hiyo. Katibu wa mahakama hiyo, Saleh Ali Abdallah, aliyasema hayo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya leseni ya baa mbalimbali za wilaya hiyo. Alisema ni jambo la kawaida wananchi kulalamikia baa zinazoanzishwa lakini wanapotakiwa kufika mahakamani kuwasilisha pingamizi hawajitokezi. Aidha, alisema mahakama pekee haina mamlaka ya kumfungia mtu ama kuizuia leseni ya baa, badaa yake inafanya hivyo baada ya wananchi kulalamika. Alisema licha ya jitihada zinazochukuliwa na mahakama hiyo katika kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari na masheha ili wananchi wajitokeze kuwasilisha pingamizi, wamekuwa hawafanyi hivyo. ...
Oman kuimarisha uwanja wa ndege Zanzibar

Oman kuimarisha uwanja wa ndege Zanzibar

Biashara & Uchumi, Nyumbani
OFISA Mtendaji Mkuu wa viwanja vya ndege vya Oman, Sheikh Aimen Ahmed Al-Hosni, amesema serikali ya Oman imeamua kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za uimarishaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, ili ufikie vigezo vinavyohitajika kimataifa kama ulivyo wa Muscat. Alisema hatua hiyo ina lengo la kuimarisha biashara ya usafiri wa anga na kuifanya Zanzibar kituo cha kiziunganishi nchi mwambao wa Afrika Mashariki na mataifa mbali mengine duniani. Alisema hayo wakati akiongoza ujumbe wa viongozi sita katika mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Vuga mjini Unguja. Alisema Oman imejitolea kuisaidia Zanzibar katika ujenzi wa uwanja huo kwa kadri ya mahitaji yaliyopo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano na uhu...
Dk. Shein kuzindua mradi kudhibiti kansa

Dk. Shein kuzindua mradi kudhibiti kansa

Jamii, Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kuchunguza kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake, unaotarajiwa kufanyika kesho. Akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Mnazimmoja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Asha Abdalla Ali, alisema hafla hiyo inatarajiwa kufanyika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul-wakil Kikwajuni. Alisema mradi huo unatekeleza kwa ushirikiano kati yao na hospitali ya Nanjing Drum Tower ya China. Alisema mradi huo wa miaka minne una lengo la kupunguza ugonjwa wa kansa ya shingo ya kizazi nchini. Hivyo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchunguza ugonjwa huo ili kupata tiba mapema kama watagundulika kuwa nao.     CHANZO: ZANZIBAR LEO
Serikali yapata hasara ya 250m/- kuvuja kwa mitihani

Serikali yapata hasara ya 250m/- kuvuja kwa mitihani

Jamii, Nyumbani
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma, amesema mtu yeyote ambae atabainika kuhusika na uvujishaji wa mitihani, atachukuliwa hatua. Aliyasema hayo katika ukumbi wa elimu mbadala Rahaleo, wakati akizungumza na watendaji wa baraza la mitihani Zanzibar. Alisema sababu ya kukutana na watendaji hao ni kutokana na kuonekana kushindwa kusimamia vyema mitihani ya kidato cha pili na kusababisha kuvuja. Alisema tukio la kuvuja mitihani limeisababishia hasara kubwa serikali ambapo zaidi ya shilingi milioni 250 zimepoteza. Alisema mbali na kutia hasara serikali imesababisha hasara kwa wazee na wanafunzi. “Mtihani ni roho ya nchi endapo tutaivujisha tutakuwa na taifa legelege ambalo litashindwa kuzalisha wataalamu hapo baadae,” alisema. Alifahamisha kuwa taarifa za
Dk. Shein: Tunaendelea kuchukua juhudi kupambana na maradhi

Dk. Shein: Tunaendelea kuchukua juhudi kupambana na maradhi

Afya, Jamii, Nyumbani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza mikakati inayochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupambana na maradhi yakiwemo ya miripuko ambapo yanapozuka huathiri watu wa rika zote wakiwemo watoto. Dk. Shein aliyasema hayo jana Ikulu, wakati alipokuwa na mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Maniza Zaman, aliyefuatana na Mkuu mpya wa shirika hilo Zanzibar, Maha Damaj, ambaye alifika kujitambulisha kwa Rais. Alieleza kuwa miongoni mwa juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ni pamoja na kujenga mitaro mikubwa ambayo itaisadia kuondosha maji yanayotuama ambayo husababisha maradhi. Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi cha mradi huo, t...
error: Content is protected !!