News Bulletin

ZATU wampongeza Rais Shein kwa agizo lake

ZATU wampongeza Rais Shein kwa agizo lake

News Bulletin
Chama cha Walimu Zanzibar zatu kimesema  utekelezwaji wa agizo   alilolitoa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein juu ya kulipwa walimu wa Zanzibar malimbikizo yao ya uzowefu wa miaka 30 ya kufanyakazi imewapa hamasa na ari walimu kuzidisha kasi ya kufundisha wanafunzi. Akizungumza na Waandishi wa habari Katibu Mkuu wa chama hizo Mussa Omar Tafurwa amesema zoezi la ulipwaji wa madeni ya walimu yameshaanza kulipwa kwa walimu pemba  na kuwaomba watendaji kuzidisha kasi ya ulipaji wa madeni hayo kwa walimu wa unguja ili na wao waweze kufaidika na fedha hizo. Tafurwa amesema ulipaji huo wa madeni umeleta faraja kwa walimu kwani kazi wanayoifanya ya kuwafundisha watoto ni kubwa na inataka umakini mkubwa hivyo  serikali iyone haja ya kuona umuhimu wa kuwalipa madeni yao wanayodai.
Usiku wa Miraj

Usiku wa Miraj

News Bulletin
Kwa mujibu wa dini ya kiislamu usiku wa Miraj ni usiku ambao Mtume Muhammad(SAW) alialikwa na Mwenyezi Mungu na kupelekwa katika mbingu saba na malaika Jibril. Mtume Muhammad(SAW) alipelekwa kutoka msikiti wa Masjid al-Haram hadi Masjid al-Aqsa na baadae kupelekwa mbinguni. Usiku huo ni usiku muhimu kwa waislamu kwani Mwenyezi Mungu alimpa Mtume Muhammad(SAW) amri kumi na mbili muhimu.
Tanzania ina mabalozi tisa kutoka Zanzibar

Tanzania ina mabalozi tisa kutoka Zanzibar

News Bulletin
NA FATINA MATHIAS, DODOMA WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema Tanzania ina  balozi 40  nje ya nchi na kwamba mabalozi wanaotoka Zanzibar ni tisa sawa na asilimia 22.5. Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk.Suzan Kolimba alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi(CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua balozi zote za nje ya Tanzania zipo ngapi na Zanzibar ina mabalozi wangapi. Dk. Kolimba akijibu swali hilo, alisema Tanzania ina  balozi 40  nje ya nchi huku mabalozi wanaotoka visiwani  Zanzibar wakiwa tisa sawa na asilimia 22.5. Katika swali la msingi, Mbunge wa Wingwi(CUF), Juma Kombo Hamad alitaka kujua Zanzibar ina nafasi gani katika Jumuiya za Kimataifa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa T
Mteule wa Rais Trump ahojiwa na Baraza la Seneti

Mteule wa Rais Trump ahojiwa na Baraza la Seneti

News Bulletin
Mike Pompeo Mteule wa Rais Donald Trump katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA), anahojiwa Alhamisi na kamati ya Seneti ikiwa ni hatua ya kuthibitishwa kwake, ambapo ataweka mkazo juu ya msimamo mkali dhidi ya Russia. “Russia imeendeleza uchokozi, fursa walioichukua kutokana na kuwepo sera dhaifu dhidi ya uchokozi huo. Hiyo ni mwisho sasa,” Pompeo ataiambia kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti, kwa mujibu wa nukuu za ushuhuda wake. Korea Kaskazini na Iran zinategemewa kuwa ni sehemu ya mazungumzo hayo Alhamisi. Kutofautiana kati ya Rais Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Rex Tillerson kulipelekea kufukuzwa kwa waziri huyo mwezi Machi. Lakini Stephen Pompeo wa Kikundi cha Kukabiliana na Migogoro
MKUTANO WA CHAMA CHA WANANCHI CUF NA WAANDISHI WA HABARI WAFANYIKA ZANZIBAR.

MKUTANO WA CHAMA CHA WANANCHI CUF NA WAANDISHI WA HABARI WAFANYIKA ZANZIBAR.

News Bulletin
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  CUF Mussa Haji Kombo katikati akifafanua baadhi ya maswala mbalimbali ya Mwenendo na Migogoro ndani ya  chama hicho kwa  Waandishi wa Habari  Mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja.kulia yake ni Kiongozi wa Ulinzi wa CUF Thney Juma na Kushoto ni  Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame. Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  CUF Mussa Haji Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari   kuhusiana na mwenendo na migogoro ndani ya Chama hicho Mkutano uliofanyika   katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja. Mratibu wa Mkutano wa CUF Ali Makame akitoa maelezo kuhusiana na Mkutano  na kumkaribisha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini  CUF Mussa Haji Kombo kuzungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Unguja
error: Content is protected !!