Mikoani

DC JOKATE MWEGELO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MUHOGO KIJIJI CHA KITANGA, KISARAWE

DC JOKATE MWEGELO AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MUHOGO KIJIJI CHA KITANGA, KISARAWE

Mikoani
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amepongeza jitihada za akinamama katika kubuni miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Serikali iko tayari kuunga mkono jitihada zao, na hasa katika miradi ya kilimo ambayo inaleta uhakika wa chakula. DC Mwegelo amesema hayo leo, Jumamosi, Septemba 15, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe, ambacho kinamilikiwa na akinamama wapatao 30 wanaoongozwa na Ofisa Kilimo mstaafu, mama Abia Magembe. Mkuu huyo wa wilaya aliweka jiwe hilo la msingi kwa niaba ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe. Alisema anapongeza jitihada kubwa zilizofanywa na akinamama hao siyo tu katika kubuni miradi ya maendel...
Watuhumiwa wa mauaji watatu wauawa kwa kuchapwa risasi na Polisi mkoani Rukwa

Watuhumiwa wa mauaji watatu wauawa kwa kuchapwa risasi na Polisi mkoani Rukwa

Mikoani
Watu watatu walioshikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa, kwa tuhuma za kufanya mauaji ya watu sita kwa kuwakata mapanga na mashoka wameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi hao baada ya kuruka katika gari la polisi na kutaka kukimbia. Tukio hilo lilitokea Septemba 20, mwaka huu majira ya saa 5 usiku katika Barabara ya Nkundi kuelekea Kijiji cha Kate, wilayani humo. Akitoa taarifa ya tukio hilo mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwataja waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi kuwa ni Nching’wa Njige (44), Dashina Ngeseyamawe (46) ambao ni wakazi wa Kijiji cha Ntalamila pamoja na Joseph Jiuke(34) mkazi wa Kijiji cha Chonga. Alisema watu hao walikuwa wamepakiwa kwenye gari la polisi ili waende kuonesha watuhumiwa wenzao ambao waliku
MV Nyerere: Rais Magufuli asema dereva aliyepaswa kuendesha MV Nyerere hakuwepo

MV Nyerere: Rais Magufuli asema dereva aliyepaswa kuendesha MV Nyerere hakuwepo

Mikoani
Sasa imebainika kwamba nahodha wa kivuko cha MV Nyerere kilichozama Alhamisi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 130 hakuwepo katika feri hiyo wakati ilipozama. Akihutubia taifa siku ya Ijumaa jioni rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa ana habari kwamba nahodha huyo alimwachia zamu ya kuendesha chombo hicho mtu ambaye hakuwa amepata mafunzo ya kazi hiyo. Akizungumza moja kwa moja kupitia runinga, rais Magufuli amesema kuwa nahodha huyo tayari amekamatwa na polisi . Aidha rais Magufuli ameagiza wale wote wanaohusika na operesheni za kivuko hicho kukamatwa ili kuhojiwa.   Na gari la wagonjwa linalotumiwa kupeleka miili ya walioopolewa hospital Kulingana na Magufuli huenda sababu ya kuzama kwa chombo hicho ni 'kujaa kupitia kiasi'. Lakini a...
Tanzania yatangaza siku nne za maombolezo

Tanzania yatangaza siku nne za maombolezo

Jamii, Mikoani
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ametangaza siku 4 za maombolezo kuanzia Ijumaa kufuatia ajali ya Ferri ya MV Nyerere kuzama katika ziwa Victoria siku ya Alhamisi. Katika ajali hiyo watu zaidi ya 130 wamethibitishwa kupoteza maisha kufikia Ijumaa, huku wengine zaidi ya 40 wakiwa tayari wamesha okolewa. Serikali imesema zoezi hilo la uokoaji linaendelea. Taarifa za awali zinaeleza kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba mizigo na abiria wengi zaidi ya uwezo wa Ferri hiyo. Serikali tayari imetuma wachunguzi katika eneo la tukio la ajali hiyo kufanya uchunguzi wa kina. Rais Magufuli ameagiza watendaji wa Kivuko na wengine wote wakamatwe katika hali ya uchunguzi huo, akiwemo kapteni wa meli hiyo. Shirika la habari la Reuters liliwanukuu maafisa wa serikali ya Tanzania waki...
error: Content is protected !!