Michezo

Nadi Ikhwan Safaa kufanya uchaguzi Sept.29

Nadi Ikhwan Safaa kufanya uchaguzi Sept.29

Michezo
BAADA ya kupita zaidi ya miaka 10 bila ya mabadiliko ya uongozi, hatimaye klabu kongwe ya muziki wa taarab asilia visiwani Zanzibar, Nadi Ikhwan Safaa, inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa wiki hii. Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Hassan Yahya, amethibitisha kwamba uchaguzi utafanyika Jumamosi ya Septemba 29, mwaka huu katika makao makuu ya klabu yaliyopo Kokoni mjini Unguja kuanzia saa 3:00 asubuhi. Hata hivyo, hadi anatoa taarifa hiyo, watu watakaosimamia uchaguzi huo walikuwa hawajawekwa bayana. Alizitaja nafasi zitakazogombewa kuwa ni Mwenyekiti na msaidizi wake, Katibu, Msaidizi Katibu, Mshika Fedha na Naibu wake, Meneja wa klabu na msaidizi, Mkurugenzi muziki na wasaidizi wawili, pamoja na wajumbe wawili wa kamati tendaji. Yahya aliwaomba wanachama wajitokeze kwa wingi na k...
Luka Modric ateuliwa mchezaji bora wa kiume Fifa, Deschamps kocha bora

Luka Modric ateuliwa mchezaji bora wa kiume Fifa, Deschamps kocha bora

Michezo
Luka Modric mchezaji bora wa Fifa Kiungo wa kimataifa wa Croatia Madrid Luka Modric,ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Fifa wa kiume katika shughuli ya utoaji tuzo iliyofanyika usiku huu London Uingereza. Modric mwenye miaka 33, amewapiga kumbo mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, anayechezea Juventus, kwa sasa pamoja na winga wa Liverpool Mohamed Salah. Marta Vieira da Silva, ametwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara sita Kwa upande wa wanawake mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Orlando Pride, Marta Vieira a Silva, ndie aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Fifa na kuwa ni tuzo yake wa sita ya uchezaji bora akiwazidi Dzsenifer Marozsan na Ada Hegerberg. Kocha wa mabingwa wa kandanda duniani Ufarasansa Didier Deschamps ameibuka kidedea kuwa ndie ko...
Uturuki yailaza Argentina katika mechi  za kombe la dunia la basketball ya wanawake

Uturuki yailaza Argentina katika mechi za kombe la dunia la basketball ya wanawake

Michezo
Uturuki imeilaza  timu ya basketball ya wanawake katika mechi ya kombe la dunia  la basketball la wanawake  ambalo linaendelea katika visiwa vya Kanari nchini Uhispania. Uturuki imeichapa Argentina 63 kwa 37 Jumamosi  katika kundi B. Baada ya ushindi  huo, timu ya basketball  ya wanawake  itachuana na timu ya Nigeria Jumapili. Timu ya Uturuki ni miongoni mwa timu 16 ambazo zinagombea kombe la dunia la basketball la wanawake ambalo litamalizika Septemba 30. Timu zinazogombea kombe hilo ni Korea Kusini, Ugiriki, Kanada, Ufaransa, Uturuki , Australia, Argentina, Nigeria, Japan, Porto Rico, Ubelgiji , Uhispania, Marekani , Senegal, China , Lettonia.     CHANZO: TRT
UONGOZI wa Malindi, umemteua Abulghan Himid Msoma,  kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu.

UONGOZI wa Malindi, umemteua Abulghan Himid Msoma, kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu.

Michezo
UONGOZI wa Malindi, umemteua Abulghan Himid Msoma,  kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu. Akizungumza na gazeti hili huko katika kiwanja cha mazoezi Mnazimmoja Unguja, Mwenyekiti wa Malindi, Mohamed Abdalla Mohamed, alisema, wamemuongeza kocha huyo kusaidiana kazi na kocha wengine waliopo kwa ajili ya kukisuka kikosi hicho. Alisema, awali timu hiyp ilikuwa ikongozwa na kocha mmoja ambae alikuwa na majukumu mawili ya kuwafundisha makipa na wachezaji jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwa kocha huyo. Mwenyekiti huyo, alisema, kocha huyo mkuu atakuwa na wasaidizi wawili ambao ni Saleh Machupa na Othman Shoka ili kufikia malengo wanayoyatarajia ya kufanya vizuri kwenye ligi hiyo. Kwa upande wake, kocha Machupa, alisema, ujio wa kocha huyo ume
Balozi Seif kufunga bonanza la Ujamaa leo

Balozi Seif kufunga bonanza la Ujamaa leo

Michezo
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa Bonanza la Ujamaa Cup , unaotarajiwa kufanyika majira ya saa 10:00 katika uwanja wa Amaan. Bonanza hilo maalum liliandaliwa kwa ajili ya kusherehekea miaka 61 tangu kuanzishwa kwa Ujamaa SC ambapo lilizishirikisha timu nane za madaraja tofauti visiwani hapa. Miamba hiyo ni pamoja na Taifa ya Jang’ombe, Malindi, Mlandege, Kundemba, Gulioni City,Raska Zone,Mchangani na Muembeladu. Katika bonanza hilo timu zote nane shiriki zilicheza kwa hatua ya makundi kwa ajili ya kupatikana washindi. Katika fainali hiyo, mshindi wa kwanza na wa pili watakabidhiwa makombe, huku timu zote shiriki zikipewa vyeti kwa ajili ya kushiriki bonanza hilo. Akizungumzia bonanza hilo kwa ujumla, Katibu wa U
error: Content is protected !!