Local

Habari Maelezo waifyagilia Mtandao wa PembaToday

Habari Maelezo waifyagilia Mtandao wa PembaToday

Local
Imeandikwa na Mohd khalfan , Pemba Mkuu wa Idara habari maelezo Pemba, Marzouk Khamis Sharif amewataka vijana kuutumia mtandao wa mawasiliano wa Pemba Today kufuata taratibu na misingi bora ili kuepuka kusambaza habari zenye kuchafua sifa ya Taifa. Amesema mitandao ya habari ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa, hata hivyo ni wajibu wa jamii kuitumia teknologia hiyo kwa manufaa badala ya hasara. Mazrouk ameyasema hayo huko ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kuhusu kuanzishwa mtandao wa vijana wa Pemba unaoitwa Pemba Today. Amesema kwamba iwapo vijana hawatakuwa na tahadhari ya matumizi ya mitandao kutasababisha kuporomoka maadili sambamba na kuchafua mila, silka na tamaduni za Taifa. Vijana kisiwani Pemba, wameanzisha mtandao wa ...
Ziara ya Balozi wa China Nchini katika hospitali ya Abdalla Mzee Pemba

Ziara ya Balozi wa China Nchini katika hospitali ya Abdalla Mzee Pemba

Local
  BALOZI wa China nchini Tanzania Wang Ke, akikagua baadhi ya maeneo ya Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, wakati alipotembelea Hospitali hiyo katika ziara yake Kisiwani Pemba.(PICHA NA HABIBA ZARALI, PEMBA) BALOZI wa China Nchini Tanzania Wang Ke, akimuangalia mmoja ya watoto waliofika katika sehemu ya mapokezi ya watoto kwa ajili ya kupata matibabu, katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani katika ziara yake Kisiwani Pemba.(PICHA NA HABIBA ZARALI, PEMBA) BALOZI wa China Nchini Tanzania Wang Ke, akimuangalia Mtoto Harithi Suleiman Hamad mwenye umri wa mwaka mmoja, aliyeathirika Mfupa wa mguu, ambapo kwa sasa mtoto huyo yuko katika hali ya uwangalizi wa madaktari wa kichina na wazalendo.(PICHA NA HABIBA ZARALI, PEMBA) BALOZI wa China Nchini Tanzania Wang K...
Makondakta wa gari za abiria acheni kupandisha bei za nauli kiholela

Makondakta wa gari za abiria acheni kupandisha bei za nauli kiholela

Local
Madereva   Wilaya ya  Wete wanaochukua abiria wa melini  Mkoani wete wametakiwa kuacha tabia ya kupandisha bei kiholela na badala yake wasubiri bei ambazo zitatangazwa na serekali kisheria. Hayo yamelezwa na katibu tawala Wilaya ya Wete Mkufu Faki Ali wakati  akizungumza na Madereva hao  jana hapo Ofisini kwake Wete. Amesema kumekua na malalamiko mengi kutoka kwa abiria juu ya nauli walioziweka  Mkoani, Wete jambo ambalo sio utaratibu uliowekwa kisheria. Aidha amesema wanaopaswa kupandisha bei za abiria ni wizara  husika inayoshughulikia masuala ya usafirishaji ndio wenye mamlaka ya kutangaza bei mpya na sio jambo  jema  kukaa madereva kuweka bei mpya kinyume na sheria . Nao madereva hao wamesema changamoto kubwa inayopelekea kufanya hivo ni kutokana na upandishwaji  wa  
Shaba FC : kifuatacho sasa ni kichapo tu kwenda mbele

Shaba FC : kifuatacho sasa ni kichapo tu kwenda mbele

Local, Sports
PICHA KUTOKA MAKTABA MTANDAO: Beki wa timu ya Shaba Hassan Suleiman, akikimbilia mpira huku mchezaji wa timu ya Mtende Rangers, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Grand Malt. Imeandikwa na Salim Hamad , Pemba BAADA ya Kufanya vyema Klabu ya Shaba FC katika mchezo dhidi ya FSC , hatimae nahodha wa timu hiyo Abdalla Salum Abdall ametamba kuwa  sasa ni mwendo wa kutoa dozi tu kwenye michezo inayosalia ili kuhakikisha inatinga hatua ya Nane bora na hata kutwaa ubingwa msimu huu. Shaba ilitoa kichapo  cha mabo 2-1 FSC katika mfululizo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba, mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani Visiwani hapa. Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kumalizika kwa mchezo  huo Nahodha huyo alisema kiu yao ni kuona timu yao inaingia kwenye hatua ya Nane bora itakashiriki
Mambo motomoto uwanja wa Gombani Pemba.

Mambo motomoto uwanja wa Gombani Pemba.

Local, Sports
  WACHEZAJI wa Timu ya ZECO wakisalimiana na wachezaji wa ZAWA wakati wa mchezo wa Mei Mosi yaliyoanza kutimua vumb I lake katika uwanja wa michezo Gombani, ZECO kuibuka na ushindi wa bao 4-1.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) MKUFUNZI wa waamuzi Kisiwani Pemba na mwamuzi wa FIFA mstaafu Ali Juma Salim katikati, akiwa katika picha ya Pamoja na waamuzi chipkizi wanaochezaji ligi za madaraja mbali mbali Kisiwani hapa, kabla ya kuanza kwa mashindano ya Mei mosi ambapo ZECO iliibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya ZAWA.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA). MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akisalimiana na wachezaji wa timu ya ZAWA, kabla ya kufungua rasmi mashindano ya Mei Mosi yaliyofanyika uwanja wa Gombani, ZECO kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya ...
error: Content is protected !!